Rais John Magufuli amesema hawezi
kuingia mgogoro wa Halmashauri ya Babati Mkoani Manyara inayoongozwa na Chadema
kulalamikia kunyang'anywa stend na CCM.
Rais Magufuli aliyasema hayo kwenye
eneo la Bicha Wilayani Kondoa mkoani Dodoma wakati akizinduzi barabara ya lami
ya Babati-Dodoma yenye urefu wa kilometa 251.
Alizungumza hilo mara baada ya mbunge
wa jimbo la Babati Mkoani Manyara Paulina Gekul (Chadema) kumuomba Rais
Magufuli aagize CCM iwarudishie stendi iliyokuwa inaingiza mapato ya
halmashauri ya mji wa Babati.
Rais John Magufuli amesema hawezi
kuingia mgogoro wa Halmashauri ya Babati Mkoani Manyara inayoongozwa na Chadema
kulalamikia kunyang'anywa stend na CCM.
Rais Magufuli aliyasema hayo kwenye
eneo la Bicha Wilayani Kondoa mkoani Dodoma wakati akizinduzi barabara ya lami
ya Babati-Dodoma yenye urefu wa kilometa 251.
Alizungumza hilo mara baada ya mbunge
wa jimbo la Babati Mkoani Manyara Paulina Gekul (Chadema) kumuomba Rais
Magufuli aagize CCM iwarudishie stendi iliyokuwa inaingiza mapato ya
halmashauri ya mji wa Babati.
Aliwataka wananchi wa mikoa inayopita
barabara hiyo waitunze ili iweze kudumu kwa miaka mingi zaidi na kuwanufaisha kiuchumi.
Alimpongeza Rais mstaafu wa awamu ya
nne Jakaya Kikwete kwa kuweka jiwe la msingi barabara hiyo wakati Rais Magufuli
akiwa Waziri wa ujenzi.
"Nakumbuka wakati huo wabunge wa
eneo hili Nkamia na mama Zabien Mhita ambao niliwaomba waniunge mkono kwa
kupisha bajeti ili barabara ijengwe," alisema Rais Magufuli.
Waziri wa Ujenzi Profesa Makame
Mbarawa alisema barabara hiyo ni miongoni mwa eneo la barabara kuu ya kaskazini
yenye kilomita 10, 228 kutoka jiji la Cape Town nchini Afrika kusini hadi jijini
Cairo nchini Misri.
Waziri Mbarawa alisema barabara hiyo
imegharimu kiasi cha sh378 bilioni, ambapo serikali ya Tanzania imetoa sh107
bilioni, benki ya maendeleo ya Afrika (ADB) sh203 bilioni na shirika la
maendeleo la Japan (Jica) sh67 bilioni.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander
Mnyeti akizungumza kwenye uzinduzi huo alisema awali wananchi wa eneo hilo
walikuwa wanatumia siku nzima kusafiri kati ya Babati hadi Dodoma ila hivi sasa
wanaotumia muda wa saa mbili.
"Hivi sasa mtu anaweza kwenda
Dodoma na kurudi Babati hata mara tatu na pia anaweza kutumia usafiri wa bajaji
kwa kutumia barabara hii," alisema Mnyeti.
Alimpongeza Rais Magufuli kwa namna
anavyoongoza nchi na kusababisha wao
wasaidizi wake kufuata nyayo zake kwa kufanya kazi kwa bidii.
Mtendaji mkuu wa wakala wa barabara
nchini (Tanroads) mhandisi Patrick Mfugale alisema mradi wa barabara ya
Dodoma-Babati umegharimu kiasi cha sh378 bilioni.
Mhandisi Mfugale alisema barabara
hiyo ambayo imeunganishwa na barabara kuu ya kutoka Afrika kusini hadi Misri,
itadumu kwa muda wa miaka 20 na madaraja yatadumu kwa miaka 120.
Balozi wa Japan Masaharu Yoshida
alisema kwa kushirikiana na benki ya maendeleo ya Afrika (ADB) wamewezesha
kufanikisha ujenzi wa barabara mbili nchini ambazo zote zimekamilika.
Balozi Yoshida alisema mradi mwingine
ni ujenzi wa barabara ya Tunduru, Mangaka hadi Mtambaaswala, ambayo nayo
imekamilika.
Alisema mradi wa barabara hiyo
ulikamilika Octoba 2017 na ulizinduliwa
na Rais Magufuli Aprili 27 mwaka huu.
Rais wa benki ya maendeleo ya Afrika,
(ADB) Dk Akinwumi Adesina alisema jamii za vijijini zitakuwa na manufaa makubwa
ya kiuchumi kupitia barabara hiyo.
Dk Adesina alisema wasafiri na
wafanyabiashara nao watanufaika na biashara mbalimbali kwa kutumia barabara
hiyo ambayo itatumika kunyanyua uchumi wao.
No comments:
Post a Comment