Michuano ya Kurugenzi Cup 2018
iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani
Manyara, Hudson Kamoga imeendelea kutimua vumbi kwa timu ya Airport SC kuifunga
Makulusa FC mabao 3-0.
Katika
mchezo huo uliofanyika jana kwenye uwanja wa shule ya msingi Haydom, hadi
mapumziko timu ya Airport SC ilikuwa inaongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na
Abubakary Maina dakika ya nne kwa njia ya penati.
Kipindi
cha pili timu ya Airport SC ilipata mabao mawili yaliyofungwa na mshambuliaji
hatari Emmanuel Mallo kwenye dakika ya 50 na ya 55.
Kwenye
mchezo mwingine timu ya Stand United timu ya Mlimani FC iliifunga bao 1-0 na
kuiondoa kwenye michuano hiyo.
Fainali
ya mashindano hayo iliyoshirikisha timu 10 inatarajiwa kufanyika jumapili ya
wiki hii kwenye viwanja hivyo vya Haydom.
Katibu
wa chama cha soka wilaya ya Mbulu (MBFA) Joseph Nicodemus alisema michuano hiyo
itakuwa chachu kwa vipaji vipya vya wilaya hiyo kupiga hatua kwenye mchezo
huo.
Nicodemus alisema anatarajia timu zitakazoshiriki michuano ya ligi daraja la tatu ngazi ya wilaya zitapata wachezaji kwenye michuano hiyo ya Kurugenzi Cup 2018.
No comments:
Post a Comment