Sunday, 27 May 2012

KAMANDA

Kamanda

KAMANDA NASARI


Kwanza kabisa namshukuru Mungu kwa kunijalia kuwa mbunge kwani nilikuwa na maono ya tangu siku nyingi kuwa mbunge wa Jimbo hili,pia nakishukuru chama changu cha CHADEMA kwa kunipa ridhaa ya kugombea na pia kwa nafasi ya pekee kwa kweli nawashukuru sana watu wa Arumeru Mashariki ambao hawakujali umri wangu,hawakujali uwezo wangu kifedha,hawakujali historia ya familia yangu katika siasa,hawakujali kila mapungufu ambayo nilikuwa nayo,lakini wakaamua kunichagua….Najua walikuja wengi na fedha nyingi,najua walikuja wengi na majina makubwa,najua walikuja wengi na kila aina ya mbwembwe,walikuja wengi na bendi nyingi za muziki,walikuja wengi wakahonga sana,walikuja wengi wakanitukana sana,walikuja wengi wakanisema sana…Lakini hatimaye sauti ya wengi imekuwa sauti ya Mungu na lile alilolipanga Mwenyezi Mungu limekwenda kutimilika,tangu mwanzo nilisema tunaanza na Mungu tunamaliza na Mungu….Walipoambiwa kuwa mimi ni mdogo kiumri wakasema siendi Bungeni kupeleka mvi au kupeleka miaka na tena wakasema wanahitaji dogo janja na siyo kubwa jinga…..Walipoambiwa kuwa mimi sijaoa wakasema siendi Bungeni kusuluhisha ndoa,walipoambiwa sina kitambi wakasema siendi kucheza mieleka Bungeni na walipoambiwa mimi ni masikini wakasema tunamuhitaji masikini mwenzetu…Narudia tena kama nilivyosema mwanzo tumeanza na Mungu na tunamaliza na Mungu….Kamanda Joshua Nassari mara baada ya kutangazwa kuwa Mbunge Mteule Jimbo la Arumeru Mashariki Aprili 2 mwaka huu.

Friday, 25 May 2012

MAKAMU WA RAIS

Makamu wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilal katika mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika nchini Botswana

DC SIMANJIRO

Mkuu wa wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara,Peter Toima akihojiwa na waandishi wa habari mara baada ya kula kiapo

Thursday, 10 May 2012

KAMANDA

Kwenye siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani nikiwa na Kamanda wa polisi mkoani Manyara Kamishna Msaidizi Liberatus Materu Sabas

PICHA

Mti wa pesa eneo la Chandama wilaya ya Chema mkoani Dodoma

Tuesday, 8 May 2012

VIJANA WAHAMISHA TAWI LA CHAMA
Na Joseph Lyimo
KATIKA tukio ambalo halikutarajiwa vijana zaidi ya 50 waliokuwa
wanachama wa CCM Tawi la Cairo Mji mdogo wa Mirerani Wilayani
Simanjiro Mkoani Manyara wameishusha bendera ya Tawi hilo na
kuipandisha ya Chadema.

Tukio hilo lilitokea juzi,baada ya wakereketwa hao kushusha bendera

hiyo na ghafla wakajiunga kwenye ufurukutwa kwa kudai kuwa CCM
imepoteza dira na mwelekeo hadi kusababisha maisha kuzidi kuwa magumu
na mfumuko wa bei.

Wakizungumza na waandishi wa habari,vijana hao walidai kuwa baadhi ya

viongozi wa CCM wa Tawi hilo wanaendesha shughuli za chama hicho
kibabe hivyo wameamua kuwaachia chama chao na kujiunga na chama cha
wajanja.

Walisema pia wamehamaka baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM mkoani

Arusha James Ole Millya kuhamia Chadema hivyo na wao wanafuata nyayo
zake kwani chama hicho ni chama makini chenye kujali watu wanyonge.

Baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo walishangazwa na kitendo hicho

kwani walidai kuwa hawajawahi kuona bendera ya chama ya Tawi
ikishushwa na kuwekwa ya chama kingine zaidi ya bendera za kwenye
mashina na siyo Tawi.

Hata hivyo,Mwenyekiti wa CCM Tawi la Cairo,Sifael Saitore aliwataka

wanachama wa eneo hilo kutokata tamaa na kutetereka kutokana na
kitendo hicho kwani huo ni upepo tu na utapita na kutulia kama
ilivyokuwa awali.

“Hata hivyo sisi hatuna jengo la ofisa ila tuna kiwanja ambacho

tunategemea kujenga ofisi na hapo mahali ofisi yetu ilipokuwa kabla
Chadema hawajaweka tawi lao ni eneo la chini ya mti wa Cairo bar na
siyo ofisi,” alisema Saitore.

Alisema hawezi kuzuia utashi na mtazamo wa vijana hao kuweka bendera

ya Chadema kwani kila mtu ana uhuru wa kufanya jambo analolitaka na
hawezi kulazimisha mtu ale wali wakati anataka kula ugali.

Alisema hivi sasa wana mikakati ya kutafuta eneo lingine kwa ajili ya

kuweka ofisi yao kwani eneo la awali lilikuwa siyo mali ya chama ni
mali ya mtu binafsi hivyo wanatafuta eneo lingine kabla ya kujenga
ofisi yao ya kudumu.

MWISHO.


VIONGOZI MJI WA MIRERANI WAPANDA MITI 200


Na Joseph Lyimo

ILI kuunga mkono jitihada za Makamu wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilal za
uhifadhi wa mazingira nchini,viongozi wa mji mdogo wa Mirerani
Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara wamepanda miti 200 ya kustawisha mji
huo.

Akiongoza zoezi hilo la upandaji wa miti juzi,Mwenyekiti wa Mamlaka ya

mji huo,Albert Siloli amesema miti hiyo imepandwa kwenye maeneo
tofauti ikiwemo taasisi mbalimbali za Serikali.

Siloli aliongoza upandaji miti akiwa na Makamu Mwenyekiti wake,Hussein

Msokoto,Mwenyekiti wa Kairo,Wilbert Nyari,Mwenyekiti wa Kilimahewa
Joseph Masasi,Ofisa Mtendaji wa mji huo,Nelson Msangi na Ofisa
Mtendaji wa kata ya Endiamtu Edumund Tibiita.

Alisema walipanda miti 30 shule ya msingi Tanzanite,miti 20 shule ya

sekondari Mirerani Benjamin Mkapa,miti 20 shule ya msingi
Endiamtu,miti 50 kituo cha afya,miti 30 ofisi ya Tarafa,na miti 20
sokoni na miti 30 kwenye nyumba za watumishi.

“Hivi karibuni tulikaa kikao cha Baraza la Mamlaka ya mji mdogo na

kuazimia kila kaya ipande miti isiyopungua 10 na kamati za vitongoji
zitasimamia zoezi hilo ili kuhakikisha mazingira ya mji yanakuwa
mazuri,” alisema Siloli.

Alisema nia na madhumuni ya zoezi hilo ni kuhakikisha kauli mbiu ya

kuufanya mji mdogo wa Mirerani unakuwa wa kijani unafanikiwa na lengo
hilo linatimizwa kutokana na mwitikio wa jamii na viongozi wao.

“Pia kwenye kikao hicho tuliazimia kuwa kila taasisi ya Serikali

iliyopo mji mdogo wa Mirerani ihakikishe kuwa inapanda miti 30 kwa
ajili ya kuunga mkono zoezi hili la kuufanya mji wetu una kuwa wa
kijani,” alisema Siloli.

WAFUGAJI NA WAKULIMA WALILIA ARDHI KWENYE KATIBA

Na Joseph Lyimo
WAKAZI wa Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara wamedai kuwa Katiba ya sasa
inawabana wananchi wa vijijini juu ya umilikishwaji ardhi hivyo katiba
mpya inatakiwa kutoa kipaumbele  cha umilikishwaji ardhi kwa wakulima
na wafugaji.

Hayo yamesemwa juzi na wakazi wa wilaya hiyo kwenye kongamano la
mchakato wa Katiba mpya lililoandaliwa na Mtandao wa Asasi za kiraia
wilayani Kiteto (KCS Forum) na kufadhiliwa na The Foundation For Civil
Society.

Mratibu wa asasi ya Naadutaro,Lembulung Ole Kosyando alisema katiba
iliyopo hivi sasa ina upungufu mkubwa wa suala la umilikishwaji ardhi
kwa jamii japokuwa katiba hiyo imeeleza kwamba ardhi ni mali ya umma.

Kosyando alisema sheria ya ardhi namba nne inazungumzia juu ya ardhi
ya miji na sheria namba tano ya ardhi inazungumza vijiji lakini sheria
hiyo namba nne kila wakati imekuwa kikwazo kwa kuimeza sheria namba
tano.

“Wananchi wa vijijini,wakulima na wafugaji hawana uhakika na matumizi
ya ardhi yao kwani kila mara sheria namba nne ya ardhi ya miji
inakinzana nao na kuwafanya wafukuzwe au kuhamishwa kwenye ardhi yao,”
alisema Kosyando.

Naye,Katibu wa UVCCM wilaya ya Tanga mjini,Gerald Augustino alisema
watanzanita wanatakiwa kujengewa uwezo kuhusu suala la ardhi kwani
rasilimali hiyo ndiyo urithi pekee wa maisha yao

“Katiba mpya inatakiwa kulinda kipengele cha ardhi kwa wananchi ambayo
ndiyo utajiri wao kwani bila kutoa kipaumbele kwenye ardhi hawatakuwa
na uhakika wa maisha yao,” alisema Augustino.

Naye,Mratibu wa KCS Forum,Nemence Iriya alisema lengo la kuandaa
kongamano hilo ni kuwaweka tayari wakazi wa wilaya hiyo ili Tume ya
kukusanya maoni ya katiba mpya itakapofika wapate cha kuzungumza.

“Kupitia kongamano hili mtakuwa tayari kutoa maoni yenu na mtatambua
nini cha kuzungumza mara baada tume ya katiba mpya itakapowafikia na
elimu mliyoipata hapa mkaieneze kwa wenzenu ambao hawakufika,” alisema
Iriya.

Pia,aliwataka wakazi hao watambue kuwa maoni ya Katiba mpya
yaliyotolewa kwenye kongamano hilo yatapelekwa kwenye tume hiyo
kupitia mjumbe wao Humphrey Polepole ambaye anaziwakilisha asasi
zisizo za kiserikali.

MWISHO.
https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/?ui=2&ik=1a30618b74&view=att&th=1372ba9369fdbf05&attid=0.3&disp=inline&realattid=87bb8472c8db62ec_0.3&safe=1&zw&saduie=AG9B_P8OncucFtZSIpKKSlSobF_A&sadet=1336471367074&sads=sRLoTdlGphB5pF3OWrO_ok_5x98
Mkurugenzi wa Tanzanite Foundation Kampuni tanzu ya TanzaniteOne Hayley Henning akimpa zawadi ya mpira mwanafunzi wa shule ya msingi New Vision iliyopo mji mdogo wa Mirerani Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara

Naisinyai

https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/?ui=2&ik=1a30618b74&view=att&th=1372ba9369fdbf05&attid=0.1&disp=inline&realattid=87bb8472c8db62ec_0.1&safe=1&zw&saduie=AG9B_P8OncucFtZSIpKKSlSobF_A&sadet=1336471201695&sads=4H0Xhl5-CdKWqm_nsfBA7CKkGTw&sadssc=1
Ofisa mahusiano msaidizi wa kampuni ya TanzaniteOne Mosses Komba akiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Oloshonyokie kata ya Naisinyai waliotembelewa na wageni kutoka nchi Marekani

Na Joseph Lyimo

WAKAZI wawili wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara wameifikisha Mahakamani Halmashauri ya Mji wa Babati wakiitaka iwalipe fidia ya zaidi ya sh78 bilioni kwa madai ya kutaifisha maeneo yao bila kuwalipa fidia kwa muda wa miaka saba iliyopita

Wakazi hao wa mjini Babati Bruno Ngomuo na Idd Ngomuo wamefungua kesi hiyo jana Jumatatu katika Mahakama ya Ardhi Wilaya  ya Babati wakisimamiwa na wakili maarufu mkoani humo Westget Lumambo.


Kwa mujibu wa hati ya madai iliyofunguliwa Mahakamani hapo mjini Babati mbele ya Mwenyekiti wake Prosper Makundi walalamikaji hao wameitaka Mahakama hiyo iwahalalishie wamiliki hao maeneo hayo.

Imedaiwa kuwa kwa muda huo wote wamekuwa wakiahidiwa kulipwa fidia lakini hakuna utekelezaji wowote uliofanyika kwa takribani miaka saba.


Hati hiyo ilieleza kuwa tangu mwaka 2004 Halmashauri ya Mji wa Babati ilitaifisha maeneo ya jumla ya ekari nne na robo mali ya Bruno Ngomuo na Idd Ngomuo na kuyagawa maeneo hayo kwa watu wengine bila kuwalipa wao fidia ambayo ni haki yao ya msingi.

Walalamikaji hao wanadai kuwa kwa muda wote huo wamekuwa wakiahidiwa kulipwa fidia lakini hakuna utekelezaji wowote uliofanyika kwa takribani miaka saba hadi hivi sasa.


Hata hivyo kwa pande wa Halmashauri ya Mji wa Babati ambao ndiyo wadaiwa katika kesi hiyo wanasimamiwa na Mwanasheria wa halmashauri hiyo Reginald Mtei. 

Shauri hilo limeahirishwa hadi Juni 20 mwaka huu ambapo upande wa wadaiwa ambao ni Halmashauri ya mji wa Babati pamoja na wadai ambao ni Bruno Ngomuo na Idd Ngomuo wametakiwa kuleta utetezi wao.


MWISHO.

Kondoa

Wafanyabiashara wa vitafunwa wa eneo la Songolo wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma

Joseph Lyimo,Simanjiro

WAKAZI wa kijiji cha Kimotorok Kata ya Loiborsiret Wilayani Simanjiro
Mkoani Manyara wamelalamikia kitendo cha walinzi wa hifadhi ya
Mkungunero kufanya ujangili wa kuwinda wanyamapori kijijini hapo na
kuuza wilayani Kondoa.

Wakizungumza na waandishi wa habari juzi,wakazi hao wamedai kuwa
walinzi hao wameanzisha mtindo huo na kisha kuwasingizia wakazi wa
kijiji hicho kwamba ndiyo wanaohusika na kuwinda wanyamapori kwenye
hifadhi hiyo.

Akithibitisha kutokea kwa vitendo hivyo Diwani wa kata ya
Loiborsiret,Lucas Ole Mukus alisema walinzi hao wamekuwa wakiwinda
wanyamapori na kuuza kisha huwasingizia baadhi ya wakazi wa kijiji
hicho kuwa ndiyo wamehusika.

Ole Mukus ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Manyara alisema hivi
karibuni gari la hifadhi hiyo aina ya Land Rover TDI lenye namba za
usajili STK 3629 lilikutwa na ngozi na nyama ya pundamilia wawili
waliowinda kwa wizi.

“Mhifadhi wa wilaya ya Simanjiro Saigurani Mollel alifuata nyayo za
gari hilo na kubaini likiwa na nyara hizo za Serikali na hadi hivi
sasa zimehifadhiwa kwa Mwenyekiti wa Kijiji hicho Melau Kunyae,”
alisema Ole Mukus.

Aliongeza kuwa walinzi wa hifadhi hiyo pia waliwakamata watoto wawili
waliokuwa wanachunga mifugo yao na kuwasingizia kuwa walikuwa
wanawinda na kutaka kuwapeleka mjini Babati kwa ajili ya kuwashtaki
mahakamani.

“Nitahakikisha suala hili nalifuatilia kwa nguvu zote kwani walinzi
hao ndiyo wangepaswa kusimamia ulinzi hifadhini hapo lakini wanafanya
uhalifu kwa kuwinda na kuwasingizia wananchi wangu,” alisema Ole
Mukus.

Hata hivyo,mmoja kati ya kiongozi wa hifadhi ya Mkungunero ambaye
hakupenda kutaja jina lake kwa vile siyo msemaji alisema matukio
yanayofanywa na watumishi wa hifadhi hiyo walishayasikia.

Alisema watumishi wote wanaotuhumiwa wameshapata majina yao na hivi
sasa uongozi wao unayafanyia kazi kabla ya kuwachukulia hatua kali
walinzi wote na madereva ambao wanahusika na matukio hayo.

MWISHO.
TanzaniteOne Mining, Ltd. Hosts
Special Guests of the Arusha International Gem Fair

By Joseph Lyimo
Mirerani Hills, Tanzania, May 2012 While attending the Arusha International Gem and Mineral Fair last week, a delegation of International visitors spent the day at the TanzaniteOne Mining operation in Mirerani, Tanzania.    Amongst the select few were Doug Hucker, AGTA, Robert Weldon, GIA, and Steve Bennett, GemsTV. 

It was an opportunity to see first hand how Tanzanite is mined at one of the world’s most sophisticated colored gemstone operations.  As guests of TanzaniteOne Ltd, and the Tanzanite Foundation, the delegation got to experience the underground operation, plant and sorthouse, as well as the Tanzanite Foundation Community Projects.  Children at a local orphanage and Primary School received gifts of soccer - and basketballs donated by Master Gemstone Carver Naomi Sarna.

Doug Hucker, CEO of AGTA, (The American Gem Trade Association), says “ We were delighted to have an opportunity to visit the Tanzanite One operation while attending the Arusha International Gem, Jewelry & Minerals Fair.  Our trip into the mine was an experience that helped us appreciate what it takes to coax these magnificent treasures from the earth.  I was especially gratified to see the work that was being done in local communities to improve the living conditions of Tanzanian children.” 


TanzaniteOne Mining Ltd:
TanzaniteOne Ltd is the world's largest and most scientifically advanced extractor and supplier of rough Tanzanite. Their unique position allows it to support and influence the entire Tanzanite chain, from mine to market.

Tanzanite:
Tanzanite, the rare and precious blue-violet gemstone, is one of the most intriguing and desirable treasures of modern times. It is found in only one place on earth, and experts agree that the chances of tanzanite being found anywhere else in the world are less that one in a million.  Its single source and finite supply mean that tanzanite is at least 1000 times more rare than diamonds. 

The color of tanzanite is so unusual  - it varies from deep dark blues to flattering shades of violet and periwinkle, pale blue, and mauve, especially in the smaller sizes.  Depending on how a stone has been cut, it will appear either more blue or violet.  Flashes of burgundy and cerise can be seen in the larger stones.  

The Tanzanite Foundation:
A non-profit, trade organization dedicated to promoting and protecting tanzanite, The Tanzanite Foundation exists to strengthen and maintain confidence in tanzanite’s integrity, educate consumers on quality and rarity, and grow value for all participants in a dynamic tanzanite market.

At the heart of their activities, The Tanzanite Foundation has sought to develop a tanzanite industry free from exploitation that truly benefits local Tanzanian communities.  To date, the Tanzanite Foundation has built two schools, a medical clinic and a community center, and pumps fresh water daily into the local community outside the tanzanite mining area.  A reverse osmosis plant has also been installed to prevent the local children’s teeth from turning brown from too much fluoride. 

Mti wa pesa uliopo eneo la Chandama wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma

Wednesday, 2 May 2012

Wanafunzi wa shule ya msingi Ngarenaro wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara wakishiriki maandamano ya siku ya wafanyakazi