Friday 31 January 2014

MBENGE ALIA KUFANYIWA FUJO


Sakata la Mbunge wa Viti maalumu wa Mkoa wa Manyara, (Chadema) Pauline Gekul kudai kufanyiwa vurugu na Mkurugenzi wa Mji wa Babati, Omary Mkombole na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Mohamed Farah limechukua sura mpya baada ya mbunge huyo kufungua kesi polisi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Gekul alisema amefungua kesi namba 606/2014 polisi Babati ya shambulio, kudhalilishwa, kuporwa fedha sh5 milioni na kufanyiwa fujo na viongozi hao wawili wa mji huo.
Alidai kuwa viongozi hao walimfanyia vitendo hivyo ikiwemo kumchania blauzi wakati wakimpokonya nyaraka zilizoonyesha uchakachuaji wa majina ya watu wanaodai fidia kwenye shamba la katani la Siratu kwenye kikao cha kamati ya Mipango na Mazingira.

“Nimefungua kesi na tutakutana Mahakamani kwani huo ni udhalilishaji wao ni wanaume na mimi mwanamke isitoshe mimi nina hadhi ya kidiplomasia sipekuliwi hovyo hovyo,” alisema Gekul.

Hata hivyo, Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara alithibitisha jana kuwa mbunge huyo kufungua malalamiko yake kwenye kituo cha polisi Babati na wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Kwa upande wao, Farah na Mkombole kwa mujibu wa taarifa yao kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana wamekanusha vikali kumfanyia fujo, kumdhalilisha na kumpora fedha mbunge huyo.

Taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkombole imedai kuwa chanzo cha kumnyanganya Gekuli nyaraka hizo ni tabia yake ya kuondoka nazo na kuzitumia kwenye vyombo vya habari na kwenye mikutano ya wananchi.

“Amefanya kosa kuondoka na nyaraka kwani ni kinyume na kanuni ya 51 ya vikao vya ndani vya kamati mbalimbali isipokuwa vikao vya Baraza tu na wananchi na vyombo vya habari wanaruhusiwa kuingia” alisema Mkombole.

Alisema awali, wajumbe wote wa kamati ya Mipango miji na mazingira ambapo Gekul ni mjumbe walitii agizo la kurudisha nyaraka kasoro mbunge huyo peke yake alitaka kuondoka nazo.

“Juhudi za kumshawishi arudishe nyaraka hizo zilishindikana kwani aligoma ndipo Mwenyekiti wa halmashauri akamnyanganya nyaraka hizo kumkabidhi Mkurugenzi na hapakuwa na purukushani wala hakupigwa wala kuchukuliwa chochote,” alisema Mkombole.

Alisema kuwa Gekul ni mjumbe halali wa vikao vya halmashauri ya mji huo na anataarifiwa na kuhudhuria mchango wake mjini Babati ila anawajibika kama kiongozi kutii na kulinda heshima kwa viongozi na wananachi anaowawakilisha.

Mbunge wa huyo wa Viti Maalumu wa Chadema wa Mkoa wa Manyara, Paulina Gekul alidai kushambuliwa na Mkurugenzi wa Halmashari ya Mji wa Babati, Omari Mkombole na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Mohamedi Fara, wakigombea kabrasha lenye majina ya wanaopaswa kupewa ardhi zilizokuwa kwenye mkoba wake.

Tukio hilo la kushambuliwa kwa mbunge huyo lilitokea juzi saa 12 jioni katika ukumbi wa halmashauri ya mji wa Babati, mara baada ya kikao kilichokuwa kikifanyika chini ya mkurungenzi huyo kumalizika.

Akizungumza mara baada ya kutoka polisi jana kutoa maelezo juu ya vurugu hizo, Gekul alisema kikao hicho kilichosababisha vurugu hizo, kilikuwa kinajadili mustakabali wa ugawaji wa shamba la Sisal Plantation lenye ekari 4200.

Alisema shamba hilo wakulima walilipia mwaka 2000 na Baraza la Madiwani lilikwishatoa uamuzi wa kugawanywa, lakini juzi katika orodha iliyotolewa, alibaini majina mengi yameghushiwa na walengwa wengi hawapo na baada ya viongozi wa halmashauri kubaini amegundua njama hizo, ndipo waliagiza kurejeshwa makabrasha yote.

“Mimi nilikataa kwa sababu orodha hii ina makosa na mimi nawafahamu baadhi ya wakulima wanaopaswa kupewa eneo hili “alisema Gekul.

Alisema Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Mohammedi Fara
baada ya yeye kukataa kurejesha, aliahirisha kikao na walipotaka kutoka nje ghafla alitokea Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Omari Mkombole ambaye alidai alikwenda Polisi kufuatilia suala la wakulima hao na tayari wanataka kuendesha msako wa waliovamia eneo hilo bila idhini ya halmashauri.

“Lakini cha ajabu baada ya kusema hivyo, mkurugenzi huyu akanifuata na kunikaba kwa nguvu, kisha kunichania nguo zangu na kunipokonya karatasi akidhani zina majina ya wakulima hao,

Alisema baada ya mlango kufungwa alianza kupokonywa kwa nguvu pochi yake na wakachambua ndani na kuondoka na nyaraka zote, huku ufunguo wa gari ukitupwa.


Tuesday 28 January 2014

KIKAO RCC MANYARA



Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Elaston Mbwilo akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 20 wa Kamati ya Ushauri ya mkoa huo (RCC) mjini Babati.



Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Kapteni Mstaafu George Huruma Mkuchika akizungumza kwenye Mkutano wa 20 wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Manyara mjini Babati.

TUNACHANGIA HOJA KIKAONI



Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Mkoani Manyara, Vrajilal Jituson akizungumza kwenye mkutano wa 20 wa Kamati ya Ushauri ya mkoa huo, ambapo alisema sheria ya manunuzi inatakiwa ibadilishwe.


Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Manyara, Pauline Gekul akizungumza juzi kwenye mkutano wa 20 wa Kamati ya Ushauri ya mkoa huo, ambapo alisema viongozi wanatakiwa kujali utawala bora wenye kufuata sheria.