Friday 27 December 2013

TUNAUKARIBISHA MWAKA 2014



Happy Kayumbo anawatakia heri ya mwaka mpya wa 2014



Gift na Andrew wanawatakia heri ya mwaka mpya wa 2014



Mireranitanzanite.blogspot inawatakia heri ya mwaka mpya wa 2014




Gift na Andrew wanawatakia heri ya mwaka mpya wa 2014

Tuesday 24 December 2013

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI KWENYE MACHIMBO YA MADINI YA TANZANITE



Wachimbaji wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilaya ya Simanjiro Mkoa wa Manyara wametaka kuchukua tahadhari kwenye migodi yao wakati wakifanya shughuli zao za uchimbaji madini hayo.

Inadaiwa kuwa baadhi ya migodi hiyo ya Tanzanite haijafunikwa juu hivyo mchimbaji anaweza kuteleza na kuanguka mgodini au mvua kubwa ikinyesha maji yanaweza kuingia ndani ya mgodi na kusababisha athari kwa waanaApolo.

Wito huo umetolewa na Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wa mkoa huo, Mrakibu Msaidizi, Elisa Mugisha wakati akiongoza kikosi chaukaguzi wa kinga na tahadhari ya moto na majanga mbalimbali kwenye migodi hiyo.




“Tumekagua migodi zaidi ya 20 na baadhi yake tukatuka inamapungufu hivyo tumewaagiza wakamilishe mapungufu yao ili wafanye shughuli zao kiuhakika ili madhara yasiweze kujitokeza,” alisema Mugisha.

Alisema pia walifika kwenye migodi ya wachimbaji wakubwa ya kampuni ya Tanzanite Africa, TanzaniteOne na Kilimanjaro Mine ila walikagua migodi mitatu ya TanzaniteOne na kubaini kuwa wamekidhi masharti ya uchimbaji madini.






 “Sisi tunatekeleza sheria za jeshi la zimamoto na uokoaji ya mwaka 2007 na kanuni ya ukaguzi na vyeti vya usalama ya mwaka 2008 na marekebisho yake ya mwaka 2012,” alisema Mugisha.

Pia, kikosi hicho cha jeshi la zimamoto na uokoaji kilikagua vituo vya mafuta na baadhi ya majengo ya biashara, makazi na taasisi mbalimbali za Serikali zilizopo kwenye mji huo wa Mirerani.