Tuesday 12 March 2013

WANAAPOLO WA TANZANITE



Hawa ni wachimbaji wadogo wa madini ya Tanzanite (WanaApolo) wa Mji mdogo wa Mirerani Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara ambao ni kati ya zaidi ya Watanzania milioni moja wanaotegemea uchimbaji mdogo wa madini na inakadiriwa kuwa madini ya Tanzanite huingiza mapato yanayofikia dola za marekani milioni 20 kwa mwaka hapa nchini lakini soko la dunia takwimu zinaonyesha huwa mauzo ya dola milioni 500 za marekani kwa mwaka yanafanyika,kiasi ambacho ni kikubwa mno ukilinganisha na takwimu za mauzo zinazopatikana hapa nchini.

ZIARA YA KINANA CHINA



Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM,Khadija Aboud akisalimiana na  Katibu wa kitengo cha kusimamia maadili wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC),Huang Xianyao,Aboud alikuwa kwenye msafara wa viongozi wa CCM wakiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahaman Omary  Kinana na ujumbe wake walipokuwa na hafla maalum iliyofanyika katika hoteli ya Dongfang Jimbo la Guangzhou,China.



Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahman Omary Kinana akimkabidhi zawadi ya kinyango cha Kimakonde,  Katibu wa kitengo cha kusimamia maadili wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Huang Xianyao,  Kinana na ujumbe wake walipokuwa na hafla maalum iliyofanyika katika hoteli ya Dongfang Jimbo la Guangzhou,China.

WAJUMBE WA ENEO TENGEFU MIRERANI



Wajumbe wa eneo tengefu la Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara wakikagua mfereji wa D’souza ambao mwaka 2008 ulisababisha vifo vya wachimbaji wadogo 79 wa madini ya Tanzanite uliojengwa kwa gharama ya sh330 milioni wakimsikiliza Kamishna Msaidizi wa madini Kanda ya Kaskazini Mhandisi Benjamin Mchwampaka.

UKAGUZI MFEREJI


Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara,Brigedia Jenerali Cosmas Kayombo (kushoto) na Mbunge wa Jimbo hilo,Christopher Ole Sendeka wakikagua mfereji wa D’Souza wa machimbo ya Tanzanite Mirerani uliogharimu sh330 milioni ambao mwaka 2008 maji yaliyopita kwenye mfereji huo uliuwa wachimbaji wadogo 79.

UKAGUZI DSOUZA


Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara,Brigedia Jenerali Cosmas Kayombo (kushoto) na Mbunge wa Jimbo hilo,Christopher Ole Sendeka wakikagua mfereji wa D’Souza wa machimbo ya Tanzanite Mirerani uliogharimu sh330 milioni ambao mwaka 2008 maji yaliyopita kwenye mfereji huo uliuwa wachimbaji wadogo 79 huku wakimsikiliza Kamishna Msaidizi wa madini kanda ya kaskazini,Benedict Mchwampaka.