Tuesday 18 December 2012

KAMANDA SURUMBU

NAIBU Katibu Mkuu wa NCCR Mageuzi,Lawrence Surumbu Tara ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Bashnet Wilayani Babati Mkoani Manyara amejivua uanachama na kujiondoa kwenye chama hicho na kujiunga na Chadema.
Tara ambaye alikuwa diwani wa kata ya Bashnet kwa tiketi ya chama cha NCCR-Mageuzi tangu mwaka 200 hadi Desemba 17,alitangaza uamuzi huo jana mjini Babati mbele ya waandishi wa habari akiwa na Mjumbe wa Kamati kuu ya Chadema Godbess Lema na kiongozi mwingine wa Chadema Ally Bananga.

LAWRENCE

Akizungumza wakati akitoa tamko lake la kujitoa NCCR Mageuzi na kujiunga na Chadema,Tara alisema amejitoa kwenye chama hicho akiwa na sababu kuu mbili zilizosababisha yeye kuhama chama hicho.
Alizitaja sababu hizo kuwa ni baadhi ya viongozi wa NCCR Mageuzi kupendelea au kuendeleza urafiki na mfumo dhalimu wa dhuluma na maovu yanayofanywa na dola chini ya Serikali ya CCM.
Alisema kutokana na hali halisi ya kisiasa nchini ilipofika na kwa jinsi dhuluma na maovu kushamiri nchini kiasi cha kufikia watumishi na viongozi wa umma kudhulumu na kufanya maovu kwa uhuru mkubwa bila hofu ya kuadhibiwa.
“Tunahitajika chama cha siasa,kilicho makini na ambacho watanzania tunapaswa kuunganisha nguvu zetu kwa pamoja bila kutengana na kwa maoni yangu NCCR Mageuzi siyo chama cha aina hiyo,” alisema Tara.

KAMANDA TARA

Naibu Katibu Mkuu wa chama cha NCCR-Mageuzi (Bara) Lawrence Surumbu Tara ambaye pia ni Diwani wa kata ya Bashnet Wilayani Babati Mkoani Manyara (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Babati ambapo alitangaza rasmi kujivua udiwani na vyeo vyote alivyokuwa navyo NCCR-Mageuzi na kujiunga na Chadema (kushoto) ni aliyekuwa mbunge wa Arusha Godbess Lema na,Kamanda Ally Bananga.


Alisema yeye ni mmoja wa waathirika wa mfumo huo mbovu wenye dhuluma kwani alidhulumiwa ubunge kwenye uchaguzi wa mwaka 2010 na kwa bahati mbaya wizi huo wa kura unaongeza maovu.
Alisema yeye alishinda ubunge wa Jimbo la Babati Vijijini kwa kupata kura kura 32,248 na mgombea wa CCM akapata kura 30,190 lakini baadhi ya wasimamizi v wakabadilisha matokeo na kumpa mgombea wa CCM kura 32,777 na yeye 31,635.
“Kule Dareda niliibiwa kura 156 na shule ya msingi Riroda niliibiwa kura 300 na Chadema wakaibiwa kura 10 ambazo zilijumlishwa kwa CCM na akaongezea kura hewa 48 kwenye shule ya msingi Riroda namba 4 na Mwada shule ya msingi shauri moyo CCM walipewa kura hewa 400.
Alisema katika mazingira hayo amebakiwa na chaguo moja wapo kati ya kubaki ndani ya chama kisichokerwa na wizi wa kura na ambao baadhi ya viongozi wake wanaendeleza urafiki na mfumo huo uliokithiri.
“Nikaona kujitenga na kuachana na chama chenye viongozi wa aina hiyo na kutafuta chama imara ambacho hakina simile na mambo kama ya aina hio chenye kupigania haki,ukweli na ambacho kimepania utawala bora na ustawi wa watanzania,” alisema.
na,Kamanda Ally Bananga.


Wednesday 12 December 2012

BURIANI PAMPAY

Kamanda wa polisi Mkoani Manyara Akili Mpwapwa (kushoto) na mwandishi wa Radio Triple A ya jijini Arusha,Hamad Mongi wakiwa kwenye mazishi ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa Triple A marehemu Juma Hamis Pampay aliyefariki dunia juzi mjini Babati kwa ugonjwa wa saratani ya inii na kuzikwa jana mjini humo