Monday, 26 August 2013

MAJI BONGADiwani wa Kata ya Bonga, Mjini Babati Mkoani Manyara, Pasian Siay akizindua mradi wa maji ya kisima kwenye kata yake.

Monday, 19 August 2013Kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara.

KIKAZI ZAIDIKwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara.

Tuesday, 13 August 2013

JB AKIONGOZA SHUGHULI ZA MAZISHI

Msanii maarufu wa filamu Jacob Stephen JB akiongoza shughuli za mazishi ya marehemu Erasto Msuya leo kwenye mtaa wa Kairo Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara hapa anapeana majukumu na mjumbe wa kamati ya mazishi Japhary Matimbwa


MAZISHI YA MAREHEMU ERASTO MSUYA BILIONEA WA MADINI YA TANZANITEMkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Malongo ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Arusha amesema Serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwa inawashikilia wote waliohusika na mauaji ya bilionea mfanyabiashara maarufu wa madini ya Tanzanite Erasto Msuya.

Akizungumza Agosti 13 mwaka huu kwenye mtaa wa Kairo Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara katika mazishi ya Msuya yaliyohudhuriwa na umati mkubwa wa watu kutoka mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro, Malongo alisema Serikali haiwezi kukaa kimya katika suala hilo la mauaji.

Alisema wafanyabiashara aina ya Msuya wanapouawa pia uchumi nao unaondolewa kwani wanaiingizia mapato Serikali kutokana na biashara wanazozifanya kwani wanalipa kodi Serikalini.

Alidai kuwa kuanzia wiki ijayo, wanatarajia kuwafikisha mahakamani mtandao wa watu wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya mfanyabiashara huyo bilionea ambaye amezikwa jana katika mazishi ya kifahari.

“Nimeongea na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele ili akutane na wafanyabiasha na wachimbaji wa madini ya Tanzanite ili matukio ya mauaji yanayotokea kila mara yaweze kukomeshwa,” alisema Malongo.

Kwa upande wake, Naibu Waziri huyo Masele aliwatia moyo wachimbaji na wafanyabiashara wa madini ya Tanzanite kwa kushirikiana katika kipindi hiki kigumu kwani Mungu ndiye atakayelipiza kisasi hicho cha Msuya.

Naye,Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Christopher Ole Sendeka amewataka wachimbaji na wafanyabiashara wa madini ya Tanzanite kushukuru kwa kila jambo ila mtandao huo wa kuondoa roho za watu zisizo na hatia ukomeshwe.

“Biblia inasema tazama ilivyo vema na kupendeza ndugu wanapokutana karibu na kuwa pamoja hivyo kama mkuu wa mkoa wa Arusha alivyosema kazi ya vyombo vya dola ni kumaliza ukatili tusiwe na shaka” alisema Ole Sendeka.