SIASA NA SERA

2 comments:

  1. JESHI la polisi Mkoani Manyara linawashikilia viongozi wanne wa chama cha walimu nchini (CWT) mkoani humo kwa kudaiwa kushawishi,kuchochea mgomo na kuwatishia walimu ambao hawakushiriki mgomo wao ulioanza Julai 30 mwaka huu.
    Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara,Kamishna msaidizi Akili Mpwapwa alithibitisha kukamatwa kwa viongozi hao kwa kuchochea mgomo,kushawishi walimu kugoma na kuwatishia wale ambao hawakushiriki kwenye mgomo huo.

    Kamanda Mpwapwa alisema viongozi hao walikamatwa jana na aliwataja majina yao kuwa ni Katibu wa CWT mkoa wa Manyara Digna Nyaki na Mwenyekiti wa CWT wilaya ya Babati Isidore Darabe.

    Aliwataja viongozi wengine wa CWT waliotiwa mbaroni kuwa ni Mwenyekiti wa CWT wa wilaya ya Mbulu Zacharia Naal na Katibu wa CWT wilaya ya Mbulu Wenceslaus Leo Musenya.

    Alisema Nyaki na Darabe wanatuhumiwa kuchochea mgomo,kumshawishi na kumtishia mwalimu wa shule ya msingi Komoto,Theresia Sulle ambaye hakushiriki zoezi la kugoma ndipo akatoa taarifa kwenye kituo cha polisi.

    “Tunatarajia kuwafikisha mahakamani viongozi hao wa CWT kwani uchunguzi wa matukio hayo umeshakamilika hivyo tutawafikisha mahakamani wakati wowote ili wakasomewe mashtaka yao,” alisema Kamanda Mpwapwa.

    Naye,Mwenyekiti wa CWT mkoani humo Qambos Sulle ambaye alikuwa kituo cha polisi Mbulu akihangaikia kuwawekea dhamana viongozi hao aliwataka walimu wasikatishwe tamaa kwa kitendo cha viongozi hao kukamatwa na polisi.

    Sulle alisema wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa wilaya wasiwatishe walimu ambao wamegoma,kwa kuwataka maofisa elimu wa wilaya kuandika majina ya walimu walioshiriki kugoma kwani mgomo ni namna ya kutafuta haki zao.

    “Lakini pia nashangazwa na kusikitishwa na viongozi wa Serikali kuingilia mhimili wa mahakama kwani kesi yetu ipo mahakamani kwa nini wasisubiri hukumu badala yake wanawakamata viongozi wa walimu,” alisema Sulle.

    Hata hivyo,Mwenyekiti wa CWT wilaya ya Simanjiro Clement Raphael alisema viongozi wa wilaya hiyo hawajakamatwa na pia Mwenyekiti wa CWT wilaya Kiteto Bakary Kilama alisema hawajakamatwa ila walimu wanaendelea na mgomo.

    “Serikali ingesubiri uamuzi wa Mahakama kuu kitengo cha kazi ambayo ilitarajiwa kutoa hukumu ya shauri hilo leo (jana) saa nane alasiri waache kuwanyanyasa walimu kwani mgomo ni haki yao,” alisema Raphael.

    MWISHO.

    ReplyDelete
  2. MAKARANI waandamizi 816 wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara
    wamechaguliwa kushiriki mafunzo ya sensa ngazi ya Tarafa kwa ajili ya
    kujengewa uwezo wa kuendesha zoezi hilo litakalofanyika Agosti 26
    mwaka huu.

    Akizungumza jana na Mwandishi wa habari hizi,mkuu wa wilaya ya
    Simanjiro Kanali Cosmas Kayombo alisema makarani hao waandamizi 816 wa
    sensa ngazi ya Tarafa wamechujwa baada ya zaidi ya watu 2,00 wa wilaya
    hiyo kuomba nafasi hiyo.

    Kanali Kayombo alisema mafunzo hayo yatafanyika kwa muda wa siku kumi
    na yanatarajiwa kuanza Agosti 9 hadi Agosti 18 mwaka huu kwenye vituo
    vya Orkesumet,Mirerani,Terrat na Msitu wa Tembo.

    Alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwaandaa makarani hao ili waendeshe
    zoezi la sensa ya watu na makazi ambapo washiriki hao ni mchanganyiko
    wa watumishi wa Serikali na watu binafsi wenye sifa ya kuendesha zoezi
    hilo.

    Hata hivyo,Kanali Kayombo alisema atawachukulia hatua kali baadhi ya
    viongozi wa dini wanaowataka waumini wao wasishiriki zoezi la sensa
    kutokana na kipengele cha dini kutoingizwa kwenye dodoso la sensa ya
    watu na makazi.

    Alisema suala la sensa ni zoezi la kisheria na endapo mtu ana hoja
    binafsi anapaswa kuwasiliana na viongozi wa Tume ya Taifa ya mipango
    wanaohusika na sensa hiyo kuliko kuwashawishi waumini wasishiriki
    kwenye sensa.

    “Dodoso la sensa haliulizi kabila,dini wala rangi ya mtu kwani katiba
    yetu haina dini ila wananchi wake wana dini hivyo mipango ya maendeleo
    ya Serikali haihusiani na dini hivyo hoja hiyo haina mashiko,” alisema
    Kanali Kayombo.

    Alisema Serikali inaendelea kuwapa hamasa kwa watu kutoa ushirikiano
    kwa makarani siku ya kuhesabiwa itakapofika na endapo watambaini mtu
    yeyote ana hamasisha watu wasishiriki zoezi hilo watamchukulia hatua
    za kisheria.

    MWISHO.

    ReplyDelete