Tuesday, 29 November 2016

OLE MILLYA


Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Mkoa wa Manyara James Ole Millya, akiwahutubia mamia ya wakazi wa mji mdogo wa Mirerani, katika ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya jimbo hilo.

Monday, 28 November 2016

TUNACHEZA BAO


Wakazi wa Kijiji cha Loiborsoit A, Kata ya Emboreet Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakicheza mchezo wa bao kwa lengo la kujifurahisha nyakati za jioni.

MAJI KITETOWananchi wa Kijiji cha Lembapul Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara wakiwa kwenye mradi wa maji.

MAHAFALI YA PILI SHULE YA SEKONDARI MGUTWA SIMANJIRO


Meneja wa shule ya sekondari Mgutwa ya Kijiji cha Kandasikira, Wilaya ya  Simanjiro Mkoani Manyara, Monica Mlemeta akizungumza kwenye mahafali, (wa pili kushoto) ni mgeni rasmi Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga, Kazimbaya Makwega na Mkurugenzi wa taasisi ya Agape Mission International inayomiliki shule hiyo Canon Kedmon Mlemeta.


Wanafunzi 65 wa kidato cha nne wa shule ya sekondari Mgutwa inayomilikiwa na taasisi ya Agape Mission International, iliyopo Kijiji cha Kandasikira Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakiwa kwenye mahafali ya pili ya shule hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga, Kazimbaya Makwega, akimpa zawadi mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Mgutwa iliyopo Kijiji cha Kandasikira, Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Isack Chacha, kwenye mahafali ya shule hiyo, kushoto ni meneja wa shule hiyo Monica Mlemeta na wapili kulia ni Mkurugenzi wa taasisi ya Agape Mission inayomiliki shule hiyo Canon Kedmon Mlemeta.