Monday 31 July 2017

WANANCHI MONDULI JUU KUNUFAIKA NA MAJI

 Zaidi ya kaya 700 za wananchi wa Kitongoji cha Irmorijo Kijiji cha Emairete Wilayani Monduli Mkoani Arusha, waliokuwa wanatumia maji ya kwenye bwana wanatarajia kunufaika na mradi wa kusafisha maji na kuchuja maji kuwa safi uliozinduliwa Kijiji hapo. 

Awali, wananchi hao walikuwa wanatumia kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kupika, kufua, kuoga na kunywa maji hayo ya bwawa ambayo pia yalikuwa yanatumiwa na mifugo ya eneo hilo. 

 Mkurugenzi wa kampuni ya Smart Vision ya Korea, Seo Young Kim akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi alisema lengo ni jamii ya eneo hilo kunufaika na maji safi na salama yanayochujwa kupitia ubunifu wao. 

Kim alisema kwa kuanza kuwanufaisha wananchi wa eneo hilo, wanatarajia kugawa majiko rafiki ya mazingira 22 na mitambo ya kuchuja na kusafisha maji ya bwawa kuwa safi na salama 22 kwa kaya 22 zitakazowanufaisha zaidi ya watu 220. 

 Alisema Smart Vision kupitia uwekezaji wa Korea Trade-Investment Promotion Agency. (KOTRA) jamii ya eneo hilo itanufaika na na mradi huo wenye lengo la kuondokana na matumizi ya maji yasiyo safi wala salama ambayo yanasababisha magonjwa ya tumbo. 

"Jamii ya eneo hili kupitia mchungaji wa kanisa la Enyorata Daniel Vengei, walileta maombi kwetu kuwa wanatatizo la maji, hospitali na shule, ndipo tukaona tuanze kutatua hili suala la maji ndipo tukaleta mitambo hii ya kuchuja na kusafisha maji," alisema Kim. 
 She said goal of project, Smart Vision head about maasai water problem in Korea. Smart Vision developed water purifier to help maasai people overcome water problem.

Kim said now Smart Vision a Korean Environmental company launches water project ina Tanzania, hopes to expand project to other parts of Tanzania where there is lack of drinking water.

"This project was aided financially bya KOTRA (Korea Trade-Investiment Promotion Agency) who supports international business of Korean companies, specifically, the KOTRA branc in Dar es salaam gave Smart Vision immense support in order to help people suffering from lack of drinking water though the water purification project," said Kim.

She said people who helped with project is Director of Smart Vision Seo-Young Kim, Manager of Smart Vision, Hyun-Jung Chung and Purifier developer and volunteer, Andrew Chung.

Mkazi wa Kitongoji cha Emairete Rose Lemomo alisema alisema awali walikuwa wanakabiliwa na tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama lakini kupitia mradi huo wataondokana na maradhi ya tumbo yaliyokuwa yakiwakabili hasa watoto. 

Lemomo aliwashukuru wote waliohusika na kufanikisha mradi huo, kwani hivi sasa watakuwa wanachota maji bwawani na kuyachuja na kuyasafisha kupitia mitambo hiyo. 

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Irmorijo, Mirishi Songoyo alishukuru shirika la Smart Vision kwa kufanikisha mradi huo wa maendeleo ambao utainufaisha jamii ya eneo hilo walioteseka kwa muda mrefu juu ya suala la maji. 

"Tunawaomba wananchi watakaofikiwa na mradi huu kuhakikisha wanawasaidia na wale ambao bado wanasubiri kupatiwa majiko na mitambo ya kuchuja na kusafisha maji," alisema Songoyo.  

Mwalimu wa shule ya msingi Irmorijo, Stephen Laizer aliwataka wananchi wote waliofanikiwa kupatiwa mradi huo kuhakikisha wanautunza ili kunufaika nao kwa muda mrefu kwani wameteseka kwa miaka mingi kwenye tatizo la maji. 

"Wageni wanapokuja kwenu inawabidi kuwashukuru hata kama hawajaacha chochote ila hawa wametuletea teknolojia ya maji, wanaweza kutufanyia mengine mazuri," alisema Laizer. 


MIGODI MIWILI YA GEM AND ROCK NA CT YA TANZANITEONE YAFUNGWA

Sakata la kifo cha mchimbaji wa madini ya Tanzanite wa mgodi wa Gem & Rock Venture wa mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, unaopakana na kampuni ya TanzaniteOne, limechukua sura mpya baada ya mgodi huo na ule wa CT kufungiwa. 

Takribani kwa muda wa siku tano mfululizo kulikuwa na vurugu zilizotokea kwenye migodi hiyo iliyopakana huku kila upande ukituhumu mgodi mwingine kuwa unawarushia mabomu ya kutengeneza kienyeji, kupitia mitobozano iliyopo.  

Kutokana na vurugu hizo mchimbaji wa mgodi wa Gem & Rock Venture, Lembris Mbatia (22) alifariki dunia na wengine 13 kujeruhiwa baada ya kudaiwa kupigwa bomu la kutengeneza kienyeji na kulipuliwa mgodini humo na wafanyakazi wa kampuni ya TanzaniteOne.  

Kamishna msaidizi wa madini kanda ya kaskazini, Adam Juma alisema amesitishwa shughuli za uchimbaji kwenye migodi hiyo miwili ili kupisha uchunguzi ufanyike juu ya mgogoro uliopo hivi sasa. 

Juma alisema wameamua kusitisha kwa muda shughuli za uchimbaji wa madini kwenye migodi hiyo miwili ili kufanyike mazungumzo baina ya pande hizo mbili na kufikiwe muafaka wa uchimbaji salama. 

Alisema wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini, kutoka kitengo cha ukaguzi wa migodi wanatarajia kufika kwenye eneo hilo na kukagua migodi hiyo miwili kwa lengo la kupata suluhu. 

Mkuu wa wilaya hiyo, mhandisi Zephania Chaula alizitaka pande hizo mbili kukaa pamoja na kupata ili kupata suluhu ya mgogoro huo ambao umesababisha kifo cha mchimbaji mmoja na wengine kujeruhiwa. 

"Pamoja na hayo, bado nasisitiza kutotumika kwa matumizi ya mabomu ya kutengeneza kienyeji kwani nimeshaagiza polisi wawachukulie hatua kali wale wote watakaobainika kuwa wanajihusisha na vitendo hivyo viovu," alisema mhandisi Chaula. 

Alisema suala la usalama katika migodini linapaswa kupewa kipaumbele kwani endapo kutatokea matatizo kwenye machimbo hayo ya Tanzanite, shughuli za uchimbaji hazitafanyika. 

Meneja wa mgodi wa Gem & Rock Venture, Joel Saitoti alisema ni kawaida ya wafanyakazi wa kampuni ya TanzaniteOne kuteka migodi mara baada ya kupata tetesi kuwa mgodi unaopakana nao unatoa madini. 

Saitoti alisema kampuni ya TanzaniteOne inavyofanya siyo jambo sahihi kwani ni migodi mingi ya wachimbaji wadogo ambayo imedhulumiwa haki zao kwa kuporwa njia zinazotoa madini. 

"Japo tumefungiwa kwa muda katika migodi yote miwili lakini wao TanzaniteOne wanaendelea na kazi kwenye migodi yao mingine na tunasubiri tukutane nao tuzungumze ili tupate suluhu," alisema. 

Hata hivyo, meneja wa ulinzi wa kampuni ya TanzaniteOne Abubakary Yombe alikanusha vikali wafanyakazi wa kampuni yake kutuhumiwa kumuua mchimbaji wa mgodi huo wa Gem & Rock Venture, Mbatia. 

Alisema wenyewe wanafanya kazi kwenye eneo la leseni yao ila wachimbaji wa mgodi wa Gem & Rock Venture ndiyo wamewaingilia katika mtobozano na kufanyia kazi sehemu ambayo siyo ya kwao. 


"Habari zinazotolewa kuwa tunateka migodi ya wachimbaji wadogo siyo za kweli kwani wao ndiyo wanaingia ndani ya eneo letu la leseni kupitia mtobozano na serikali inapaswa kuchukua hatua juu ya hilo ili kukomesha tatizo hilo," alisema Abubakary. 

WANANCHI WA NAMALULU WATOA KERO KWA DC WA SIMANJIRO


Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mhandisi Zephania Chaula akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Namalulu Kata ya Naberera, baada ya Esupat Laizer kulalamikia changamoto ya maji, wizi wa punda na migogoro ya ardhi 

MCHIMBAJI KWENYEMADINI YA TANZANITE AFARIKI DUNIA

 Mchimbaji wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, amefariki dunia kwa kukosa hewa na wengine 13 kujeruhiwa baada ya kudaiwa kupigwa bomu la kutengeneza kienyeji na kulipuliwa mgodini kwao na walinzi wa kampuni ya TanzaniteOne. 

Pia, askari polisi wa kituo cha Mirerani walijeruhiwa na kupata majeruhi usoni, kichwani na mikononi wakati wakiingia kwenye mgodi huo kwa kukwaruzwa na miamba wakati wakikagua chanzo cha tatizo hilo. 

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi Francis Massawe alisema tukio hilo lililotokea usiku wa kuamkia Julai 29 mwaka huu. 

Kamanda Massawe alimtaja marehemu huyo kuwa ni Lembris Mbatia (22) mkazi wa Sekei jijini Arusha, ambaye mwili wake umehifadhiwa kwenye hospitali ya rufaa ya mount Meru. 

Alisema kuna baadhi ya wafanyakazi wa mgodi huo walioishiwa hewa na kupandishwa mgodini kisha wakapelekwa hospitali kupatiwa huduma ya kwanza. 

"Bado tutafanya uchunguzi wa tukio hilo ila chanzo ni mtobozano wa mgodi huo na mgodi wa CT unaomilikiwa na kampuni ya TanzaniteOne," alisema kamanda Massawe. 

Mkuu wa wilaya hiyo, mhandisi Zephania Chaula aliwataka wachimbaji hao kuwa watulivu kipindi hiki cha kuondokewa na mwenzao na wengine kujeruhiwa baada ya kutokea tatizo hilo. 

"Ninyi ni wangu na TanzaniteOne ni wangu mimi ndiyo baba yenu hivyo nimesikiliza malalamiko yenu ila fanyeni subira tunafanya kikao na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya na kamishna msaidizi wa madini na RPC yupo tutatoa maamuzi," alisema mhandisi Chaula. 


Kamishna Msaidizi wa madini kanda ya kaskazini, mhandisi Adam Juma alisema hawezi kuongea chochote hadi hapo watu wote waliopo kwenye migodi hiyo miwili wapandishwe juu ndiyo ataweza kutoa tamko lolote. 

"Bado nafanya mawasiliano na kamishna wa madini mhandisi Benjamini Mchwampaka, juu ya tukio hilo hivyo vuta subira nitatoa tamko juu kinachofuata," alisema Juma. 

  
Hata hivyo, meneja ulinzi wa kampuni ya TanzaniteOne, Abubakary Yombe alisema hawezi kuzungumza chochote kwani anashughulikia suala la usalama wa wafanyakazi wake waliokuwa eneo la tukio. 

"Tufanye mawasiliano baadaye kwani nazama kwenye mgodi wa CT kuangalia mambo yanavyokwenda nitaongea na waandishi wa habari nikipanda juu, " alisema Yombe huku akijiandaa kuzama kwenye mgodi huo. 

Meneja wa mgodi huo wa Gem & Rock wenye PML namba 0002333 Joel Saitoti alisema mgogoro na kampuni hiyo ndiyo umesababisha hali hiyo kwani walitumia mtobozano na mgodi wa jirani yao kufanya fujo. 

Saitoti alisema wao hawajatobozana nao kwani wanafanya kazi sehemu yao ila waliposikia hali ya mgodi ipo vizuri wakawafanyia fujo na kusababisha matatizo hayo. 

DC BABATI AWAPA ELIMU WANANCHI WA LUXMANDA JUU YA MATUMIZI YA MAJI

 Mkuu wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Raymond Mushi akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Luxmanda Kata ya Secheda, juu ya mgogoro wa maji (kushoto kwake) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Hamis Malinga.

MHESHIMIWA ANNA GIDARRYA:HATUTETEI WEZI MALI ZA UMMA TUNAKWEPA KUENDELEA KUACHIWA MAGOFU KWENYE MACHIMBO YA MADINI


ASEMA WANAOSEMA UPINZANI WANATETEA WEZI NI SIASA ZA MAJI TAKA. 

Wananchi wametakiwa kupuuza habari mbalimbali za kizushi zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ambazo zinaeleza kuwa vyama vya upinzani vinapinga juhudi za maendeleo na kutetea wezi wa mali za umma wakiwemo mafisadi.

Kauli hiyo ameitoa Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Manyara Anna Gidarya akizungumza kwenye uzinduzi wa albamu ya kwaya ya Ukombozi ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na umati na Usharika wa Haydom Mtaa wa Bethania. 

“Kuna watu wamekuwa wasemaji wakuu kwenye mitandao ya kijamii huwenda nyie watu wa Bethania hamuingii sana kwenye mitandao kulingana na mazingira ya huku watu wanasema wapinzani wamekuwa wakimpinga Rais John Magufuli hatupingi juhudi zozote za rais tunachotaka upinzani hatutaki kurejea miaka 54 iliyopita kuingia katika mikataba mibovu inayopelekea nchi yetu kutofaidika na rasilimali zilizopo wawekezaji wamekuja wamechimba madini yetu wametuachia mashimo hatutaki kuendelea kuwa hivyo tuanataka mambo yaende sawa sawia na si kupinga maendeleo yoyote ya nchi,” alisema Gidarya.

Aliwataka wananchi wilayani mbulu na mkoa mzima wa Manyara kutokukubali kuendelea kutokuamini habari za mitandao ya kijamii zinzozushwa ikiwemo kile alichoeleza kuwa habari zenye udini ili kuepeuka kuliingiza taifa katika uvunjifu wa amani na umoja wa  Taifa.

“Ndugu zangu kuna watu wengine wanasmabaza habari ambazo zina udini nawaombeni tusifanye siasa kwenye mioyo ya waliowengi na tutaishia pabaya manona yanayoendelea kibiti kuna watu wanahusisha na udini hatuna uhakika nawaombeni ndugu zangu habari za namna hii kwamba kuna kiongozi anazungumzia masuala ya udini naombeni mzipuuze ni siasa chafu ambazo hazina ishara nzuri kwa taifa letu,” alisema Gidarya.

Kwa upande mwingine Mmbunge huyo ameiasa jamii  hususan wananchi wa mkoa wa Manyara kuhifadhi chakula kilichopatikana kutokana na hali mbaya ya hewa ili kuodnokana na kukumbwa na baa la njaa siku zo usoni.
“Kina mama uzuri hapa leo hatuzungumzi kwenye majukwaa na hapa tunazungumza na watu wanao mjua Mungu watu wa bethania kila mmoja anajua Mama mzuri na baba mzuri kila awae mzazi mnajua mzazi mzuri ni Yule anayekumbuka kuhifadhi akiba ya chakula kwaajili ya familia yake hifadhini chakula serikali haina hata maghala haina chakula cha akiba kugawa kwa wananchi wake itakapotokea njaa,” mheshimiwa Anna Gidarya alisema.

Mheshimiwa Anna pia amewahimiza akina mama na vijana kufika katika ofisi za halmashauri zao kuuliza juu ya utaratibu wa asilimia hamsini ambazo zinatengwa kwaajili ya kugawiwa vikundi vya vijana na akina mama kwaajili ya kuanzisha miradi ya kujiendeleza kiuchumi.

“Nendeni kwenye hamalshauri ulizeni hiyo asilimia ni haki yenu mfuateni diwani muulizeni pia juu ya fedha hizo awape ufafanuzi hizo fedha zipo kwa ajili ya vikundi vyenu,” alisema Gidarya.

Naye muinjilisti kiongozi wa kanisa la Bethania usharika huo wa hydom ameungana na Mmbunge huyo kwa kumshukuru kwa dhati kwa kutoa elimu hiyo na hamasa hiyo kwa vikundi kwa vijana na akina mama kwani ni jambo muhimu sana jamii kukumbushwa juu masuala hayo.

“Mheshimiwa mbunge mi niseme tu nimefurahishwa na elimu ulioitoa leo hapa kwa waumini na wananchi hawa unajua ni bora mtu akupe elimu kuliko akupe fedha jamani ndugu zangu nimefurahishwa leo na mheshimiwa Mmbunge kutoa elimu hii bora mtu akupe elimu kuliko akupe kitu kingine tukushukuru sana Mheshimiwa Mmbunge mungu akubariki” Petro Emmanuel alisema.

Katika uzinduzi wa albamu hiyo ya kisulisuli ya kwaya ya ukombozi iliyobeba myimbo kumi Mheshimiwa Mmbunge Anna Gidarrya ameweza kuchangia zaidi ya milioni sita katika kuchangia kwa hiyo kuweza kuendelea na kazi yake ya kutangaza injili kupitia nyimbo za injili.




MAGAZETI YA JUMATATU LEO JULAI 31, 2017