MICHEZO

2 comments:

  1. WASANII maarufu wa muziki wa kizazi kipya wa mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara,Wanaapolo wameibuka upya baada ya kurekodi wimbo wao uitwao Sinyorita kwenye studio za Sharobaro Records chini ya Producer Bob Junior.

    Wanaapolo ambao ni wasanii maarufu wenye uwezo wa kumiliki jukwaa wanatarajia kutoa album yao yenye nyimbo nane itakayoitwa Sinyora ambayo itarekodiwa kwenye studio tofauti za jijini Dar es salaam.

    Kwa mujibu wa meneja wa Wanaapolo,Shamila Ramadhani kundi hilo linasimamiwa kazi zake na Club Delux Mapipa ya mji huo chini ya Mkurugenzi wake Mohamed Issa (Uspime) na Thadey Chusa.

    Shamila alisema kundi la Wanaapolo linaundwa na wasanii wanne ambao ni Ramadhan Ally (Maimun) Ramadhan Mussa (Kize Bize) Omary Michael (Ben Lee) na Issa Amos (Wa2b).

    “Baadhi ya nyimbo zitakazounda albamu ya Sinyorita ambazo zinatarajiw kurekodiwa hivi karibuni zaidi ya Sinyorita yenyewe ni Homa ya mapenzi,Kazimika na Kinyulinyuli,” alisema Shamila.

    Alisema hivi sasa kundi hilo linaendelea na mazoezi makali mji mdogo wa Mirerani kwenye ukumbi wa Delux Mapipa ili baada ya mwezi huu waanze kufanya matamasha mbalimbali hapa nchini.

    “Kundi la Wanaapolo limepata umaarufu mkubwa hapa nchini kutokana na stahili yao ya kushambulia jukwaa kwa umahiri mkubwa na wa hali ya juu uliowawezesha kujulikana sehemu mbalimbali,” alisema Shamila.

    Alisema kuwa wasanii wote wa kundi hilo ni wazaliwa wa mji mdogo wa Mirerani kwenye machimbo maarufu ya madini ya Tanzanite ndiyo sababu wakajiita jina la wanaapolo.

    MWISHO.

    ReplyDelete


  2. MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Manyara Dorah Mushi amesema Serikali inatakiwa kuharakisha uanzishaji wa eneo la uwekezaji wa biashara ya nje (EPZA) uliopo mji mdogo wa Mirerani.

    Akizungumza juzi na wakazi wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro wakati alipopokelewa baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo Mushi alisema EPZA itakuwa tegemeo kubwa la Mirerani pamoja na madini ya Tanzanite.

    “Mradi wa EPZA ni tegemeo kubwa kwa wakazi wa mji mdogo wa Mirerani na Simanjiro kwa ujumla kwani fursa za uchumi zitaongezeka na kusababisha watu wasitegemee madini ya Tanzanite peke yake,” alisema Mushi.

    Alisema mradi huo ni wa muda mrefu na hatambui kikwazo kinachokwamisha kuanzishwa kwa mradi huo ambapo wakazi waliokuwa wanamiliki maeneo ya mradi huo walishakubali kuhama ili kuupisha.

    “Jamii ya Mirerani na Simanjiro itanufaika kiuchumi kupitia EPZA kwani bidhaa na mazao yatakayozalishwa na wakazi hao ikiwemo madini ya Tanzanite, Tomarini ya kijani,gaineti,mifugo,ngozi yatafanya wapige hatua,” alisema Mushi.

    Alisema ni muda mrefu sasa umepita bila eneo hilo kuendelezwa wakati ambapo ardhi ya kujengwa EPZA imeshatengwa na mji huo hivyo kusubiri Serikali kuanza kujenga eneo hilo.

    Mwenyekiti huyo alisema kuwa watu wengi hasa wanawake wa eneo hilo watanufaika kutokana na mradi huo ambao umekuwa tegemeo kubwa lakini utekelezaji wake bado haujafanyika.

    Alisema watu wamekuwa na maswali mengi kuliko majibu kuhusiana na mradi huo ambao ni tegemeo kubwa kwao lakini kupitia nafasi aliyonayo hivi saa atakuwa anawakumbusha viongozi wa Serikali juu ya hatima ya EPZA Mirerani.

    MWISHO.

    Joseph Lyimo,Mirerani

    WANYANGE 14 wanatarajiwa kuchuana kwenye mashindano ya kumtafuta Miss Utalii wa Mkoa wa Manyara unaotaraji kufanyika Octoba 12 mwaka huu kwenye ukumbi wa Kangaroo Hoteli Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro.

    Akizungumza jana na waandishi wa habari,Mratibu wa michuano hiyo Mosses Komba alisema maandalizi ya mpambano huo yameshakamilika na hivi sasa warembo hao wanafanya mazoezi kila siku kwa kupanda milima ya madini ya Tanzanite.

    Komba alisema kupitia kampuni yake ya New Vision mashindano hayo yanatasindikizwa na mwanamuziki maarufu Wanne Star anayefanya muziki wake kwa kuimba na kucheza nyimbo za asili,Morgan Sound Band na Sarakasi.

    Alisema michuano hiyo ya Miss Utalii mkoa wa Manyara inadhaminiwa na kampuni ya Ken Family General Trading Co,Radio 5,Kangaroo Hotel,Manga Gems,White Fashion,Manyara Inn na Baba G Intertainment.

    Alisema warembo watakaoshikiri mashindano hayo ni wasichana wa wilaya zote tano za mkoa huo ikiwemo Simanjiro,Kiteto,Mbulu,Hanang’ na Babati ambao ni wanyange wa kiiraq,kimasai,kibarbaig na kifyomi.

    Alitoa wito kwa watu wote wanaopendelea burudani za urembo kujitokeza kwa wingi kwenye mashindano hayo ili kuwaunga mkono wasichana hao wa mkoa wa Manyara ambao wote ni chipukizi katika masuala ya urembo.

    “Lengo la mashindano hayo ni kuutangaza utalii wa ndani wa mkoa wa Manyara na ninawapongeza wazazi wa wasichana hawa wa mkoa wa Manyara kwa kuruhusu watoto wao wa kike kushiriki mashindano hayo,” alisema Komba.

    MWISHO.

    ReplyDelete