Wednesday, 26 March 2014

HIFADHI YA TAIFA YA TARANGIRE
Nikiwa kwenye utalii wa ndani Hifadhi ya Taifa ya Tarangire Tarangire ilianzishwa Juni 19 mwaka 1970 kupitia tangazo la Serikali namba 160 likiwa na eneo la kilomita za mraba 2,850 na asilimia nane ya mfumo wa ikolojia wa Tarangire-Manyara wenye kilomita 35,000.Mkuu wa Hifadhi ya Tarangire Stephano Qolli anasema hifadhi hiyo ilianzishwa ili kuhifadhi maeneo ya mto Tarangire na ardhi oevu ambayo ni chanzo pekee cha maji katika kipindi cha kiangazi, kwani kipindi hicho kinakuwa na mkusanyiko mkubwa wa wanyama kwenye eneo hla hifadhi.Qolli anaeleza kuwa vivutio vilivyopo kwenye hifadhi hiyo ni idadi kubwa ya wanyama wa aina mbalimbali ikiwemo Tembo (nyumbani kwa tembo), mto Tarangire, Uhamaji wa wanyama kwa makundi makubwa wakiwemo nyumbu na pundamili, ardhi owevu za silale na Lamakau, ndege wa aina mbalimbali ambazo ni zaidi ya aina 550 na miti mikubwa ya mibuyu.  Kwa upande wake, Mkuu wa idara ya utalii, Beatrice Kessy anasema bidhaa za utalii zilizopo Tarangire ni utalii wa kuona wanyama kwa gari mchana, utalii wa kuona wanyama usiku, utalii wa kutembea kwa miguu, utalii wa kuruka na puto, utalii wa kupiga picha na filamu, utalii wa kupiga kambi ndani ya hifadhi na utalii wa kula chakula cha moto porini.

Saturday, 22 March 2014

PONGEZI MIRERANI BENJAMIN MKAPA KWA UFAULU MZURIWanafunzi wa shule ya sekondari Mirerani Benjamin Mkapa wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wakiwasikiliza walimu na viongozi wa Mji mdogo wa Mirerani, baada ya wanafunzi watatu kupata divishen one na mmoja kupata divishen two, tangu shule hiyo ianzishwe mwaka 2002 haijawahi kufaulisha hivyo.Mkuu wa Kituo cha polisi Mirerani, Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, SP Ally Mohamed Mkalipa akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Mirerani Benjamin Mkapa ambapo alitoa shilingi laki 3 kwa wanafunzi watatu waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka jana na kupata Divishen One.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Mirerani Benjamin Mkapa wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wakiwasikiliza walimu na viongozi wa Mji mdogo wa Mirerani, baada ya wanafunzi watatu kupata divishen one na mmoja kupata divishen two, tangu shule hiyo ianzishwe mwaka 2002 haijawahi kufaulisha hivyo.Diwani wa kata ya Endiamtu Mji mdogo wa Mirerani, Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Lucas Chimbason Zacharia akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Mirerani Benjamin Mkapa ambapo aliwapongeza wanafunzi wa watatu waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka jana na kupata Divishen One na mwanafunzi mmoja aliyepata divishen two.