Wednesday, 23 September 2015

KAMANDA UVCCM SIMANJIRO DANIEL OLE MATERI

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana akimkabidhi cheti na kumpongeza Mkurugenzi wa Grace Land Hotel Daniel Ole Materi ambaye ni Kamanda wa UVCCM Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, katikati ni Mkuu wa wilaya hiyo Mahmoud Hashim Kambona na Katibu wa CCM mkoani humo Ndeng'aso Ndekubali.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana akimkabidhi ngao Mkurugenzi wa Grace Land hotel Daniel Ole Materi na kumsimika kuwa Kamanda wa UVCCM Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara.
Kamanda wa vijana wa UVCCM Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Daniel Ole Materi akiwapungia mkono wakazi wa Mji mdogo wa Mirerani, baada ya kusimikwa na Ktibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana.

LUCAS ZACHARIA

Katibu Uchumi na Fedha wa CCM Mkoani Manyara, Lucas Chimbason Zacharia akijinadi mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Omary Kinana, kwa wakazi wa Mji mdogo wa Mirerani wakati akiomba kuchaguliwa kuwa diwani wa Kata ya Endiamtu.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahaman Kinana akimsikiliza Katibu Uchumi na Fedha wa CCM Mkoa wa Manyara, Lucas Zacharia wakati akiomba kura ili achaguliwe tena kuwa Diwani wa Kata ya Endiamtu.
Mgombea udiwani wa Kata ya Endiamtu Wilayani Simanjiro Lucas Chimbason Zacharia ambaye pia ni Katibu Uchumi na Fedha wa CCM mkoani Manyara, akiwaomba kura wakazi wa kata hiyo.

MAGUFULI BUKOBA

 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John  Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa Gymkhana mjini Bukoba tayari kuhutubia wakazi wa Manispaa ya Bukoba.

Umati wa wakazi wa manispaa ya Bukoba wakiwa wamefurika katika viwanja vya Gymkhana kumsikiliza mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Magufuli .

MTWARA MOJA

LOWASSA AWASHUKURU WANANCHI WA MASASI KWA MAPOKEZI MAKUBWA ALIYOYAPATIA

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwasili kwenye Uwanja wa Boma, Mjini Masasi Mkoani Mtwara, kulikifanyika Mkutano wake wa Kampeni za kuomba ridhaa ya wananchi kugombea nafasi, uliofanyika leo Septemba 22, 2015.


Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Masasi, Mkoani Mtwara, waliofikia kusikiliza sera zake katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Boma, leo Septemba 22, 2015. Ambapo amewashukuru wananchi wa Mji wa Masasi kwa mapokezi makubwa waliyompatia.
Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye akizungumza machache na wananchi wa Jimbo la Masasi Mjini, Mkoani Mtwara waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Boma, leo Septemba 22, 2015.CHANZO OTHMAN MICHUZI
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwapungia mkono wananchi wa Mji wa Masasi, Mkoani Mtwara, muda mfupi baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Boma, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni, leo Septemba 22, 2015.
Uwanja wa Boma mjini Masasi, palikuwa hapatishi pale Mgombea Urais alipowasili uwanjani hapo.

Mgombea wa Ubunge anaekubalika na wananchi wa Masasi kupitia Mwamvuli wa Chama cha Wananchi CUF, Ismail Makombe (Maarufu kwa Jina la Kundambada), akizungumza machache na wananchi hao waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Boma, leo Septemba 22, 2015.
Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa kupitia Chama cha NLD, Dkt. Emmanuel Makaidi akiwa ameambatana na Mkewe, wakiwasalimia wananchi wa Mji wa Masasi, Mkoani Mtwara leo Septemba 22, 2015.
Chademaaaaaa.........
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akipokea karatasi ya Shairi kutoka kwa Msoma Mashairi, Mohamed Ally (kushoto) mara baada ya kughani Shairi lake.

Magambo yenye jumbe mbali mbali.
Sehemu ya Wananchi wa Mji wa Masasi, Mkoani Mtwara wakiwa katika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Boma, leo Septemba 22, 2015.

Thursday, 17 September 2015

MAFURIKO GEITA

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akihutubia Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Stendi ya Zamani ya Chato, Wilayani Chato, Mkoani Geita  Septemba 16, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnaji Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chato, Dkt. Benedicto Lukanima, katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Stendi ya Zamani ya Chato, Wilayani Chato, Mkoani Geita  Septemba 16, 2015.
Mh. Tundu Lissu akiwasalimia wananchi wa Jimbo la Chato, Mkoani Geita  Septemba 16, 2015.
Waziri Mkuu wa zamani, Mh. Fredrick Sumaye, akihutubia Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Stendi ya Zamani ya Chato, Wilayani Chato, Mkoani Geita  Septemba 16, 2015.