Awali, wananchi hao walikuwa
wanatumia kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kupika, kufua, kuoga na kunywa maji
hayo ya bwawa ambayo pia yalikuwa yanatumiwa na mifugo ya eneo hilo.
Kim alisema kwa kuanza
kuwanufaisha wananchi wa eneo hilo, wanatarajia kugawa majiko rafiki ya
mazingira 22 na mitambo ya kuchuja na kusafisha maji ya bwawa kuwa safi na
salama 22 kwa kaya 22 zitakazowanufaisha zaidi ya watu 220.
Alisema Smart Vision
kupitia uwekezaji wa Korea Trade-Investment Promotion Agency. (KOTRA) jamii ya
eneo hilo itanufaika na na mradi huo wenye lengo la kuondokana na matumizi ya
maji yasiyo safi wala salama ambayo yanasababisha magonjwa ya tumbo.
"Jamii ya eneo hili kupitia
mchungaji wa kanisa la Enyorata Daniel Vengei, walileta maombi kwetu kuwa
wanatatizo la maji, hospitali na shule, ndipo tukaona tuanze kutatua hili suala
la maji ndipo tukaleta mitambo hii ya kuchuja na kusafisha maji," alisema
Kim.
She said goal of project, Smart
Vision head about maasai water problem in Korea. Smart Vision developed water
purifier to help maasai people overcome water problem.
Kim said now Smart Vision a
Korean Environmental company launches water project ina Tanzania, hopes to
expand project to other parts of Tanzania where there is lack of drinking
water.
"This project was aided
financially bya KOTRA (Korea Trade-Investiment Promotion Agency) who supports
international business of Korean companies, specifically, the KOTRA branc in
Dar es salaam gave Smart Vision immense support in order to help people
suffering from lack of drinking water though the water purification project,"
said Kim.
She said people who helped with
project is Director of Smart Vision Seo-Young Kim, Manager of Smart Vision, Hyun-Jung
Chung and Purifier developer and volunteer, Andrew Chung.
Mkazi wa Kitongoji cha Emairete
Rose Lemomo alisema alisema awali walikuwa wanakabiliwa na tatizo la
upatikanaji wa maji safi na salama lakini kupitia mradi huo wataondokana na
maradhi ya tumbo yaliyokuwa yakiwakabili hasa watoto.
Lemomo aliwashukuru wote
waliohusika na kufanikisha mradi huo, kwani hivi sasa watakuwa wanachota maji
bwawani na kuyachuja na kuyasafisha kupitia mitambo hiyo.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha
Irmorijo, Mirishi Songoyo alishukuru shirika la Smart Vision kwa kufanikisha
mradi huo wa maendeleo ambao utainufaisha jamii ya eneo hilo walioteseka kwa
muda mrefu juu ya suala la maji.
"Tunawaomba wananchi
watakaofikiwa na mradi huu kuhakikisha wanawasaidia na wale ambao bado
wanasubiri kupatiwa majiko na mitambo ya kuchuja na kusafisha maji,"
alisema Songoyo.
Mwalimu wa shule ya msingi
Irmorijo, Stephen Laizer aliwataka wananchi wote waliofanikiwa kupatiwa mradi
huo kuhakikisha wanautunza ili kunufaika nao kwa muda mrefu kwani wameteseka
kwa miaka mingi kwenye tatizo la maji.
"Wageni wanapokuja kwenu
inawabidi kuwashukuru hata kama hawajaacha chochote ila hawa wametuletea
teknolojia ya maji, wanaweza kutufanyia mengine mazuri," alisema
Laizer.
No comments:
Post a Comment