Miundombinu ya shule ya sekondari ya
Kata ya Loiborsiret Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, imezidi kuimarishwa
baada ya kumalizika vyumba viwili vya madarasa na nyumba sita za walimu.
Diwani wa kata ya Loiborsiret Ezekiel
Lesenga (Mardadi) aliyasema hayo wakati akizungumza kwenye sherehe ya
kuvuka rika kwa vijana wa irkiponi na kuwa wazee iliyofanyika kitongoji cha
Ndepes.
Mardadi alisema
wamemaliza kujenga madarasa hayo mawili, vyoo vyenye matundu nane na nyumba
sita kubwa zilizo pamoja zenye vyoo na bafu ambazo zitaishi familia sita za
walimu wa shule hiyo.
Alisema wanasubiri serikali kukabidhi
majengo hayo ambayo yamekamilika na bado wanaendelea kujenga mabweni ya
wavulana kwa wanafunzi wa shule hiyo ambayo hivi sasa yapo kwenye msingi.
“Baada ya awali mimi binafsi kukabidhi
madawati 100 kwenye shule hii ya sekondari Loiborsiret, naishukuru serikali ya
wilaya iliyoongeza madawati 28 mengine na hivi sasa yameshafika,” alisema
Mardadi.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Loiborsiret
Martin Noongululu alitoa wito kwa vijana waliovuka rika kuwa wazee, waendelee
kuchangia shughuli za maendeleo ikiwemo elimu kwani maendeleo hayajastaafu.
Noongululu alisema baada ya vijana hao
kutumia miaka 20 ya ujana wao kwa kushiriki shughuli za maendeleo, wanapaswa
kuendelea kufanikisha maendeleo ya eneo hilo ili eneo hilo lizidi kupiga hatua.
“Kipindi hiki cha miaka miwili
niliyooongoza kijiji hichi nimepata ushirikiano mkubwa wa maendeleo nikiwa na
vijana hawa waliovuka rika hivyo waendeleze ushirikiano walionipa,” alisema
Noongululu.
Mzee wa mila wa eneo hilo Alais Koina
alisema jamii ya wafugaji wa kimasai inawategemea wazee kwenye kutoa maamuzi
yao ya kila siku hivyo anatarajia vijana hao waliovuka rika watatimiza jambo
hilo.
“Kupitia nafasi waliyoipata hawa hivi
sasa wamekuwa wazee na jamii yetu ya kifugaji inatarajia maamuzi makubwa kutoka
kwa wazee na vijana kazi yao itakuwa ni kutekeleza maamuzi hayo,” alisema
Koina.
Asanten viongoz wetu kwa kuitupia jicho shule ya sekondari ya loiborsiret
ReplyDeleteKipekee niwashukur viongoz wetu kwa kuzid kuboresha shule yetu ya sekondari ya loiborsiret
ReplyDeleteKipekee niwashukur viongoz wetu kwa kuzid kuboresha shule yetu ya sekondari ya loiborsiret
ReplyDeleteMiaka minne zilizopita shule ya sekondari ya loiborsiret ilikuwa katika hali mbaya mno hasa kwa upande wa majengo,walimu kuwa wachache kuliko masomo na pia huduma ya maji na umeme.Lakini kwa sasa imeboreshwa zaidi baada ya viongozi wetu wa awamu ya tano kuwajibu ipasavyo katika kuongeza majengo na huduma zingine kama vile maji na umeme
ReplyDeleteNapenda kutumia fursa hii kuwapongeza viongozi wetu wakiongozwa na Diwani wa kata ya loiborsiret, Diwani viti maalum pamoja na wenyeviti wa vijiji vinavyounda kata ya loiborsiret kwa kweli wanafanya kazi hongereni sana.
Miaka minne zilizopita shule ya sekondari ya loiborsiret ilikuwa katika hali mbaya mno hasa kwa upande wa majengo,walimu kuwa wachache kuliko masomo na pia huduma ya maji na umeme.Lakini kwa sasa imeboreshwa zaidi baada ya viongozi wetu wa awamu ya tano kuwajibu ipasavyo katika kuongeza majengo na huduma zingine kama vile maji na umeme