ASEMA WANAOSEMA UPINZANI WANATETEA WEZI NI SIASA ZA
MAJI TAKA.
Wananchi wametakiwa kupuuza habari mbalimbali za kizushi zinazosambazwa kwenye mitandao
ya kijamii ambazo zinaeleza kuwa vyama vya upinzani vinapinga juhudi za maendeleo na
kutetea wezi wa mali za umma wakiwemo mafisadi.
Kauli hiyo ameitoa Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Manyara Anna Gidarya akizungumza kwenye uzinduzi wa albamu ya kwaya ya Ukombozi ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na umati na Usharika wa Haydom Mtaa wa Bethania.
“Kuna watu wamekuwa wasemaji wakuu kwenye mitandao ya
kijamii huwenda nyie watu wa Bethania hamuingii sana kwenye mitandao kulingana
na mazingira ya huku watu wanasema wapinzani wamekuwa wakimpinga Rais John Magufuli hatupingi juhudi zozote za rais tunachotaka upinzani hatutaki
kurejea miaka 54 iliyopita kuingia katika mikataba mibovu inayopelekea nchi
yetu kutofaidika na rasilimali zilizopo wawekezaji wamekuja wamechimba madini yetu
wametuachia mashimo hatutaki kuendelea kuwa hivyo tuanataka mambo yaende sawa
sawia na si kupinga maendeleo yoyote ya nchi,” alisema Gidarya.
Aliwataka wananchi wilayani mbulu na mkoa mzima wa Manyara
kutokukubali kuendelea kutokuamini habari za mitandao ya kijamii zinzozushwa
ikiwemo kile alichoeleza kuwa habari zenye udini ili kuepeuka kuliingiza taifa
katika uvunjifu wa amani na umoja wa Taifa.
“Ndugu zangu kuna watu wengine wanasmabaza habari ambazo zina udini
nawaombeni tusifanye siasa kwenye mioyo ya waliowengi na tutaishia pabaya
manona yanayoendelea kibiti kuna watu wanahusisha na udini hatuna uhakika
nawaombeni ndugu zangu habari za namna hii kwamba kuna kiongozi anazungumzia
masuala ya udini naombeni mzipuuze ni siasa chafu ambazo hazina ishara nzuri
kwa taifa letu,” alisema Gidarya.
Kwa upande mwingine Mmbunge huyo ameiasa jamii
hususan wananchi wa mkoa wa Manyara kuhifadhi chakula kilichopatikana kutokana na
hali mbaya ya hewa ili kuodnokana na kukumbwa na baa la njaa siku zo usoni.
“Kina mama uzuri hapa leo hatuzungumzi kwenye majukwaa na hapa tunazungumza na
watu wanao mjua Mungu watu wa bethania kila mmoja anajua Mama mzuri na baba
mzuri kila awae mzazi mnajua mzazi mzuri ni Yule anayekumbuka kuhifadhi akiba
ya chakula kwaajili ya familia yake hifadhini chakula serikali haina hata
maghala haina chakula cha akiba kugawa kwa wananchi wake itakapotokea njaa,”
mheshimiwa Anna Gidarya alisema.
Mheshimiwa Anna pia amewahimiza akina mama na vijana
kufika katika ofisi za halmashauri zao kuuliza juu ya utaratibu wa asilimia
hamsini ambazo zinatengwa kwaajili ya kugawiwa vikundi vya vijana na akina mama
kwaajili ya kuanzisha miradi ya kujiendeleza kiuchumi.
“Nendeni kwenye
hamalshauri ulizeni hiyo asilimia ni haki yenu mfuateni diwani muulizeni pia
juu ya fedha hizo awape ufafanuzi hizo fedha zipo kwa ajili ya vikundi vyenu,” alisema Gidarya.
Naye muinjilisti kiongozi wa kanisa la Bethania
usharika huo wa hydom ameungana na Mmbunge huyo kwa kumshukuru kwa dhati kwa
kutoa elimu hiyo na hamasa hiyo kwa vikundi kwa vijana na akina mama kwani ni
jambo muhimu sana jamii kukumbushwa juu masuala hayo.
“Mheshimiwa mbunge mi
niseme tu nimefurahishwa na elimu ulioitoa leo hapa kwa waumini na wananchi
hawa unajua ni bora mtu akupe elimu kuliko akupe fedha jamani ndugu zangu
nimefurahishwa leo na mheshimiwa Mmbunge kutoa elimu hii bora mtu akupe elimu
kuliko akupe kitu kingine tukushukuru sana Mheshimiwa Mmbunge mungu akubariki”
Petro Emmanuel alisema.
Katika uzinduzi wa albamu hiyo ya kisulisuli ya kwaya
ya ukombozi iliyobeba myimbo kumi Mheshimiwa Mmbunge Anna Gidarrya ameweza kuchangia
zaidi ya milioni sita katika kuchangia kwa hiyo kuweza kuendelea na kazi yake
ya kutangaza injili kupitia nyimbo za injili.
No comments:
Post a Comment