Hawa ni wachimbaji wadogo wa madini ya
Tanzanite (WanaApolo) wa Mji mdogo wa Mirerani Wilaya ya Simanjiro Mkoani
Manyara ambao ni kati ya zaidi ya Watanzania milioni moja wanaotegemea
uchimbaji mdogo wa madini na inakadiriwa kuwa madini ya Tanzanite huingiza
mapato yanayofikia dola za marekani milioni 20 kwa mwaka hapa nchini lakini
soko la dunia takwimu zinaonyesha huwa mauzo ya dola milioni 500 za marekani kwa
mwaka yanafanyika,kiasi ambacho ni kikubwa mno ukilinganisha na takwimu za
mauzo zinazopatikana hapa nchini.
Tuesday, 12 March 2013
ZIARA YA KINANA CHINA
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM,Khadija Aboud akisalimiana na Katibu wa kitengo cha
kusimamia maadili wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC),Huang Xianyao,Aboud
alikuwa kwenye msafara wa viongozi wa CCM wakiongozwa na Katibu Mkuu wa
CCM,Abdulrahaman Omary Kinana na ujumbe wake walipokuwa na hafla maalum
iliyofanyika katika hoteli ya Dongfang Jimbo la Guangzhou,China.
Katibu
Mkuu wa CCM,Abdulrahman Omary Kinana akimkabidhi zawadi ya kinyango cha
Kimakonde, Katibu wa kitengo cha kusimamia maadili wa Chama Cha
Kikomunisti cha China (CPC), Huang Xianyao, Kinana na ujumbe wake
walipokuwa na hafla maalum iliyofanyika katika hoteli ya Dongfang Jimbo la
Guangzhou,China.
WAJUMBE WA ENEO TENGEFU MIRERANI
Wajumbe wa eneo tengefu la Mirerani Wilayani
Simanjiro Mkoani Manyara wakikagua mfereji wa D’souza ambao mwaka 2008
ulisababisha vifo vya wachimbaji wadogo 79 wa madini ya Tanzanite uliojengwa
kwa gharama ya sh330 milioni wakimsikiliza Kamishna Msaidizi wa madini Kanda ya Kaskazini Mhandisi Benjamin Mchwampaka.
UKAGUZI MFEREJI
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara,Brigedia Jenerali Cosmas Kayombo (kushoto) na Mbunge wa Jimbo hilo,Christopher Ole Sendeka wakikagua mfereji wa D’Souza wa machimbo ya Tanzanite Mirerani uliogharimu sh330 milioni ambao mwaka 2008 maji yaliyopita kwenye mfereji huo uliuwa wachimbaji wadogo 79.
UKAGUZI DSOUZA
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara,Brigedia Jenerali Cosmas Kayombo (kushoto) na Mbunge wa Jimbo hilo,Christopher Ole Sendeka wakikagua mfereji wa D’Souza wa machimbo ya Tanzanite Mirerani uliogharimu sh330 milioni ambao mwaka 2008 maji yaliyopita kwenye mfereji huo uliuwa wachimbaji wadogo 79 huku wakimsikiliza Kamishna Msaidizi wa madini kanda ya kaskazini,Benedict Mchwampaka.
Subscribe to:
Posts (Atom)