MKUU wa Mkoa wa
Manyara, Alexander Mnyeti ameendesha harambee iliyopatikana sh17. 5 milioni ya
umaliziaji wa jengo maabara ya shule ya sekondari Bishop Hando ya Wilayani
Mbulu.
Pia, Mnyeti
amewapa zawadi ya sh1 milioni walimu wa shule hiyo na wanafunzi wakapewa
magunia 100 ya mahindi ya chakula kwa kushika nafasi ya kwanza kwenye matokeo
ya kidato cha nne mwaka 2017.
Aliendesha zoezi
hilo kwenye ziara yake ya siku saba ya kutembelea halmashauri ya wilaya ya
Mbulu ambapo atakagua na kuzindua miradi ya maendeleo na kuzungumza na
wananchi.
Mnyeti
akizungumza kwenye shule hiyo amemuagiza mkuu wa wilaya hiyo Chelestino Mofuga
kuhakikisha maabara hiyo inakamilika ndani ya muda wa miezi mitatu.
"Hata mimi
niliwahi kuwa mkuu wa shule ya sekondari, natambua gharama za ujenzi zilivyo,
hapa panahitajika sh40 milioni, sisi tumechangia sh17. 5 milioni sasa pambaneni
mlimalize jengo hili," alisema Mnyeti.
Mkuu wa wilaya
hiyo Mofuga alimuhakikishia Mnyeti kuwa atafanikisha usimamizi wa umaliziaji wa
maabara hiyo ndani ya miezi mitatu kama alivyoagiza.
"Kupitia
nafasi hii nakuagiza mtendaji wa kata ya Masqaroda na mtendaji wa kijiji
kuendesha michango kwa wananchi ili tumalize jengo hili la maabara,"
alisema Mofuga.
Awali, mwalimu wa
shule hiyo ya sekondari Bishop Hando, Samuel Surumbu alisema kiwango cha
taaluma kwa wanafunzi kinafanikiwa kutokana na ufundishaji wa walimu na kuwepo
kwa chakula shuleni.
Mwalimu Surumbu
alisema pia wanasaidiwa kufundisha na walimu wengine wa kujitolea wanaofundisha
masomo ya sayansi.
Alisema
wanakabiliwa na changamoto mbalimbali
ikiwemo wa upungufu wa majengo ikiwemo ofisi za walimu, nyumba za walimu na
bwalo la kulia chakula.
Diwani wa kata ya
Masqaroda Peter Tarmo alimshukuru Mnyeti kwa kuendesha zoezi hilo
lililofanikisha upatikanaji wa fedha hizo zitakazosaidia umaliziaji wa jengo
hilo la maabara.
"Huu mzigo
hivi sasa utakuwa mwepesi tofauti na hapo awali, tutajipanga na wananchi wangu
na wilaya yetu kuhakikisha maabara hii inakamilika," alisema Tarmo.
No comments:
Post a Comment