Saturday, 23 February 2013

RIP ASKOFU LAIZER

Maaskofu wa mbalimbali wakiaga mwili wa marehemu Dk Thomas Laizer

JK AKIHANI MSIBA



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifariji ndugu, jamaa na marafiki wa familia zilizoondokewa na watoto na wazazi kufuatia ajali ya barabarani maeneo ya kijiji cha Kibiki, Ubena Zomozi katika mkoa wa Pwani Februari 11 mwaka huu iliyoua hapohapo watu wanane wakiwemo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chalinze baada ya gari dogo aina ya Toyota Mark II lililokuwa limebeba abiria wanane kugongana uso kwa uso na roli
 

Wednesday, 20 February 2013

KAZI KWELI KWELI

1.Hata Manyunyu ni mvua
2.Tajiri hanuniwi
3.Pesa na chakula siyo vitu vya kususa
4.Heshima pesa kipara kovu tu
5.Silaha pesa bastola mzigo
6.Chezea mshahara usichezee kazi
7.Hata manyunyu ni mvua
8.Ukiona manyoya ujuwe kishaliwa
9.Ikisimama panda
10.Ukitaka utajiri sharti uamke usiku
11.Pombe pombe tuu kunywea bar mbwembwe tu
12.Mtumbwi hauna saitimira
13.Njia ya chooni haioti nyasi

MAJIVU

Paroko msaidizi wa Kanisa Katoliki,Malkia wa Rozali,Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara,Padri Modest Makiluli akimpaka majivu Gift Thadey,kwenye ibada ya jumatano ya majivu kanisani hapo kuashiria kuanza kwa kwaresma.

KULA KEKI

Mtoto Susan Tills wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara,akimlisha keki mdogo wake Brigete Tills wakati wa sherehe yake iliyofanyika Kazamoyo Resort (Kwa Mdava) baada ya kupata ubatizo na ubarikio hivi karibuni.

MAZOEZI


Mtoto Gift Thadey na Andrew Joseph wa Mji Mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara,wakiwa nyumbani kwao wakifanya mazoezi ya kulamba dole gumba la mguu huku mama yao Happy Kayumbo akiwaangalia.

Friday, 15 February 2013

MBUNGE MSIBANI

Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Mkoani Arusha,Joshua Nassari akiwana na baadhi ya wachungaji kwenye mazishi ya marehemu Boniface Gadi mchimbaji mdogo wa madini ya Tanzanite,ambaye alifariki dunia kwa kuangukiwa na ngema katika machimbo ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani na kuzikwa Mbuguni wilayani Arumeru.