Ahadi za ujenzi wa barabara
zilizotolewa na Rais John Magufuli wakati wa kampeni ya kugombea urais mwaka
2015 alipotembelea Mkoani Manyara, zipo kwenye mchakato wa utekelezaji wake.
Alisema kazi ya upembuzi yakinifu na
usanifu wa kina inaendelea kutekelezwa na mhandisi mshauri M/S Cheil
Engeneering co Ltd ya Korea kaskazini na M/S Inter-consult Ltd ya Tanzania.
Pia, utekelezaji wa miradi ya
barabara za mkoa huo zilizopo kwenye ilani ya uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) kwa mwaka 2015/2020 unafanyiwa kazi.
Meneja wa wakala wa barabara nchini
Tanroads mkoani Manyara, mhandisi Bashiri Rwesingisa aliyasema hayo kwenye
kikao cha bodi ya barabara ya mkoa huo, kilichofanyika mjini Babati.
Mhandisi Rwesingisa alisema barabara
ya Arusha-Kibaya-Kongwa, yenye urefu wa kilometa 336.6 inayopitia Losinyai
wilayani Simanjiro na Dosidosi wilayani Kiteto, inafanyiwa upembuzi na usanifu
wa kina.
Alisema kazi ya upembuzi yakinifu na
usanifu wa kina inaendelea kutekelezwa na mhandisi mshauri M/S Cheil
Engeneering co Ltd ya Korea kaskazini na M/S Inter-consult Ltd ya Tanzania.
Alisema barabara ya
Karatu-Mbulu-Haydom-Singida ya urefu wa kilometa 190 inafanyiwa upembuzi na
usanifu wa kina kupitia mhandisi mshauri M/S H.P. Gauff Ingenieure
akishirikiana na wenzake watatu.
Alisema barabara ya
Karatu-Mbulu-Haydom-Singida ya urefu wa kilometa 190 inafanyiwa upembuzi na
usanifu wa kina kupitia mhandisi mshauri M/S H.P. Gauff Ingenieure
akishirikiana na wenzake watatu.
Awali, mbunge wa jimbo la Mbulu
Vijijini, Flatei Massay akizungumza juu ya ahadi hizo za Rais Magufuli za
ujenzi wa barabara za lami, alisema bado utekelezaji haujafanyika kwenye
barabara ya Haydom kilometa tano na Dongobesh kilometa tano.
Mbunge wa jimbo la Mbulu mjini Paul
Isaay alisema ahadi ya Rais ya kilometa tano za barabara za mji wa Mbulu bado
haujatekelezwa na pia barabara ya mlima Magara bado ina changamoto kubwa.
Mbunge wa Babati mjini Pauline Gekul
alisema Rais Magufuli alitoa ahadi akiwa uwanja wa Kwaraa kuwa zitajengwa
kilometa 20 za lami, hivyo utekelezaji unapaswa kufanyika.
Mbunge wa jimbo la Simanjiro James
Ole Millya alisema Rais mstaafu Jakaya Kikwete aliagiza barabara za makao makuu
yote ya wilaya nchini iwekwe lami lakini Orkesumet hadi sasa haina hata kipande
cha lami.
Hata hivyo, mkuu wa mkoa huo,
Alexander Mnyeti alisema atahakikisha anasimamia ahadi zote zilizotolewa kwa
nyakati tofauti na viongozi hao wawili wakuu wa nchi zinatekelezwa kwa wakati.
"Najua utekelezaji ukifanyika
ipasavyo mwaka 2020 tukienda kwa wananchi ni hiyena hiyena tunachukua nchi na
wengine tunaendelea kuwa wakuu wa mikoa," alisema Mnyeti.
No comments:
Post a Comment