Rais Jakaya Kikwete akisikiliza maelezo ya namna wauguzi wanavyotoa huduma zao kwenye maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani iliyofanyika kitaifa kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha .
Rais
Jakaya Kikwete ametoa wito kwa wananchi kujitaidi kupima afya zao kwanza
ili kubaini wanaugua ugonjwa gani kabla ya kutumia dawa.
Rais
Kikwete aliyasema hayo wakati alipokuwa akihutubia katika kilele cha sherehe za
maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani ambapo kitaifa yalifanyika jana jijini
Arusha.
Alisema kuwa ni wajibu wa kila mwananchi kupima afya yake kabla ya
kunywa dawa kwani itamsaidia kujua nini au ugonjwa gani unamsumbaua
Aidha Kikwete akiongelea ugonjwa wa denguae alisema kuwa ugonjwa
huu uliongia hapa nchi ni hatari hivyo ni wajibu wa kila mtanzani
anahakikisha ana uthibiti ugonjwa huu.
alisema kuwa iwapo kila mtu atafuata mashariti ikiwa ni
pamoja na kulala ndani ya chandalua chenye dawa ,pamoja na kufukia madibwi yote
basi ugonjwa huu unaweza kutoweka kabisa .
kwa upande wa wauguzi alisema kuwa amesikia kero zao na
atazifanyia kazi kwa yale ambayo yatawezekana, badhi ya matatizo ya wauguzi
ambayo wameyataja mbele ya Rais ni pamoja na kuitaji malipo ya mazingira
hatarishi, walitaka vyeo vipandishwa kwa wakati pamoja na kulipwa malipo ya
likizo kwa wakati.
Pia waliomba ruzuku kwa masomo ya juu pamoja na kuboreshewa maeneo
ya kazi.
No comments:
Post a Comment