Mashindano ya kumsaka mrembo wa Mkoa wa Manyara, Miss Manyara 2014 inatarajia kufanyika mjini Babati May 31 mwaka huu ambapo washiriki 15 wa kutoka Wilaya za Simanjiro, Hanang’ Mbulu, Kiteto na Babati wanatarajia kushiriki.
Mratibu wa kampuni ya Mirerani Entertainment ya
mjini Babati, Akon Clement, ambao ndiyo waandaaji wa mashindano hayokizungumza na waandishi wa habari juzi alisema
maandalizi ya mashindano hayo yanaendelea vizuri.
'Hivi sasa maandalizi ya kufanyika kwa Miss Manyara, yanaendelea vizuri
kwani washiriki kutoka kwenye wilaya hizo wanaendelea na mazoezi kwa ajili ya
kupatikana kwa wawakilishi wa mkoa huo," alisema Clement.
Alisema wapo
kwenye mazungumzo na baadhi ya waadhamini waliotuahidi kutuunga mkono kwenye
Missi Manyara 2014, kwani mdhamini mkuu ni kampuni ya Tanzania Breweries kupitia
kinywaji chake cha Redds.
Alitaja
baadhi ya wadhamini wanaotarajia kudhamini Miss Manyara 2014 ni Manyara
Compyuta, Chuo kikuu huria Manyara, Motel Silver, Trimas Saloon,
Mireranitanzanite.blogspot.com , Shambani Solution Green belt na Fear Deal.
“Wadhamini
wengine wanaotarajia kutudhamini kwenye shindano letu ni Motel Silver, Tina
Classic, Pole pole Coach, San Abima Classic, Alno Technology, Ziggy Supermarket
na Code Marketing,” alisema Clement.
Alitoa
ombi kwa wazazi na walezi wa wilaya za mkoa huo, kuwapa ruhusa mabinti wao ili
waweze kushiriki mashindano hayo, kwani mabinti wa jamii za wairaqw, wadatoga,
wamasai, wambugwe na wafyomi wana uzuri wa asili.
“Pia
tunaendelea na mazungumzo na baadhi ya wasanii wakubwa wa muziki kutoka jijini
Dar es salaam na wasanii wengine chipukizi wa hapa hapa Babati na mkoa mzima wa
Manyara kwa ujumla watashiriki,” alisema Clement.
No comments:
Post a Comment