Monday, 28 April 2014

UZINDUZI, HARAMBE NA KIPAIMARA BABATI


Askofu wa Jimbo la Mbulu Mkoani Manyara, Beatus Kinyaiya akiweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa kanisa jipya la Parokia ya Roho Mtakatifu mjini Babati, linalotarajia kugharimu sh915 milioni, ambapo aliwapa kipaimara vijana 116 na kuendesha harambee na shilingi 28,322,000 zilipatikana jumapili iliyopita.

Miongoni mwa vijana 116 waliopewa kipaimara na Askofu wa Jimbo la Mbulu Mkoani Manyara, Beatus Kinyaiya jumapili iliyopita kwenye kanisa la Parokia ya Roho Mtakatifu mjini Babati.

Umati wa watu waliohudhuria kwenye kanisa Katoliki Parokia ya Roho Mtakatifu Dikonia ya Babati Mkoani Manyara, ambapo Askofu wa Jimbo la Mbulu, Beatus Kinyaiya aliwapa kipaimara vijana 116, aliweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa kanisa jipya la Parokia ya Roho Mtakatifu, linalotarajia kugharimu sh915 milioni na akaendesha harambee iliyokusanya shilingi 28,322,000.

No comments:

Post a Comment