EDWARD MORINGE SOKOINE:MZALENDO WA KWELI TANZANIA.
Alizaliwa tarehe 1 August 1938, Monduli, Arusha. Alifariki tarehe 12 April 1984 akiwa kijana wa miaka 45. Alifariki katikaajali ya Gari alipokuwa akitoka Dodoma katika shughuli za kiserikali kuelekea mjini Dar es salaam.
Alipofika maeneo ya Dakawa, Morogoro, gari alilokuwa akisafiria
liligongana na Toyota Land Cruiser iliyokuwa ikiendeshwa na ‘mpigania uhuru’ wa
Afrika Kusini, Dumisan Dube.
“NDUGU wananchi, leo saa saba mchana;ndugu yetu na kijana wetu, Ndugu
Edward Moringe Sokoine, alipokuwa safarini kutoka Dodoma kuja Dar es
salaam, gari yake ilipata ajali, amefariki dunia”.
Ni hotuba ya
Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, aliyoitoa jioni ya Alhamisi Aprili 12, 1984 na kurushwa na Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) na kusikika kila kona ya nchi, kisha kuleta vilio kwa Watanzania.
Ndugu Sokoine, amepata elimu ya sekondari kutoka Shule ya vipaji ya
UMBWE, iliyopo KIBOSHO mkoani Kilimanjaro 1958. Alijiunga na TANU
mwaka 1961 na baadae aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa
Tanzania mwaka 1977.
Alidumu katika kiti hicho kuanzia 1977 hadi 1981, tena
kuanzia 1983 hadi mauti yalipomfika 1984. Edward Moringe Sokoine, Mmaasai anaaminika
kuwa mchapa kazi na mzalendo pengine kuliko mawaziri wengi wa sasa na wa
zamani, Moja kati ya nukuu toka moja ya hotuba zake:
"Ole wake kiongozi mzembe na asiye na nidhamu nitakayemkuta: Kiongozi wa siasa hana usalama wa aina yoyote. Usalama wake ni kudra ya Mungu na Wananchi peke yake.
Viongozi wazembe na wabadhirifu wahesabu siku zao.
Labda tusiwajue. Hawa hatuna sababu ya kuwapa imani, kuwa tutawalinda kama vitendo
vyao viovu" - Edward Moringe Sokoine, 26 Machi 1983
Mwanzoni mwa vuguvugu la vyama vingi, aliyekuwa Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, Mabere Marando, aliwahi kumzungumzia Sokoine akisema ndiye kiongozi mzalendo zaidi kuwahi kutokea nchini.
Marando alisema aliwahi kuwamo kwenye msafara wa Sokoine huko Kibaha. Baada ya shughuli za siku nzima, ilipofika saatisa alasiri uongozi wa Kibaha
ukamkaribisha Sokoine na msafara wake kwenye chakula kilichoandaliwa katika moja ya shule za msingi.
Kama kawaida kiongozi akitembelea sehemu, mapochopocho huandaliwa. Siku
hiyo vyakula viliandaliwa, Kabla watu hawajaanza kujichana, Sokoine akauliza: “Hivi hawa watoto (wanafunzi) waliopo hapo nje wamenisubiri tangu saa ngapi?”
Akajibiwa kuwa tangu asubuhi ya siku hiyo. Akauliza: “Wameshakula?” Hakupata jibu. Akasema: “Mimi ninarejea Dar es Salaam na hivyo kila mtu akale kwake. Hiki chakula wapeni hawa watoto wakile.” Duh! Ilikuwa bonge la sherehe kwa watoto wakati Waziri Mkuu akiamrisha msafara uondoke. Aliyenuna akanuna, aliyecheka akacheka!
Huyo ndiye Sokoine, Waziri Mkuu aliyekuwa akiwafikiria wengine zaidi.
Waziri gani leo hii anaweza kuwaza watoto kama wamekula au hawajala?
Yaani aache kufikiria posho na marupurupu mengine!
Sidhani. Hata kifo chake inasemekana kilitokea baada
ya kukataa kupanda ndege kurejea Dar es Salaam, akaamua kupanda gari ili njiani
akague miradi
kadhaa ya maendeleo. Waziri gani anazo sifa kama zake?
kadhaa ya maendeleo. Waziri gani anazo sifa kama zake?
Wengi wanajiuliza, ingekuwa vipi Sokoine angeendelea
kuishi? Tanzania ingekuwa wapi leo?
Leo shujaa Edward Sokoine anatimiza miaka 30 tangu
atangulie mbele ya haki
Tutamkumbuka Daima.
Tutamkumbuka Daima.
When he returned from Germany, he became District Executive Officer of the Masai District, then he was elected to the National Assembly for the Masai Constituency.
In 1967 he became Deputy Minister of Communication, Transportation and Labour. The next step in his career was the promotion to the Minister of State in 1970. In 1972, he switched to the post of the Minister of Defence and National Service of Tanzania. In 1975, he was elected to the National Assembly again, this time for Monduli.
Two years later, he became a member of the Central Committee of the ruling party Chama Cha Mapinduzi (CCM). In the same year (1977) began his first term in office as Prime Minister of the United Republic of Tanzania. This term lasted till 1981.
After a year-long break, he became Prime Minister again in 1983. He stayed just one year in office, till his death in April 1984, in a car accident.
There is a university in Morogoro, Tanzania, named after him. Sokoine University of Agriculture (SUA) began in 1964 as an agricultural college offering diploma in agriculture. It was elevated to a faculty of agriculture in 1969 under the University of Dar es Salaam.
KUMBUKUMBU YA
KILA MWAKA:
Aprili 12 ya kila mwaka,
taifa limekuwa likiadhimisha kumbukumbu ya kiongozi huyo kwa kufanya shughuli
mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kuendesha makongamano, midahalo,
mabonanza, ibada, riadha na upandaji mlima Kilimanjaro.
Katika utawala wa hayati baba
wa taifa na rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwalimu Julius
Kambarage Nyerere, katika eneo la Wami Sokoine kulijengwa nyumba moja na
banda moja linalotumika kama jukwaa lakini kwa sasa majengo hayo yamechakaa,
anasema msimamizi wa eneo hilo, Hamis Said Mpandachuri.
Waandishi walifika katika
eneo hilo na kukuta mnara wa picha ya Sokoine ukiwa umepakwa rangi mpya za
manjano, kijani, blue na nyeusi huku chini ya picha yake kukiwa na maneno “Alimtumikia Mungu kwa kuwatumikia watu,
sauti ya watu ni sauti ya Mungu”.
Mbali ya mnara huo na majengo
yaliyojengwa katika utawala wa serikali ya kwanza, pia liko jengo jipya na la
kisasa ambalo linaendelea kujengwa nyuma ya majengo ya zamani.
Kwa mujibu wa uongozi wa
halmashauri ya wilaya ya Mvomero, jengo hilo ni kwa ajili ya shule ya sekondari
ya Sokoine (Sokoine memorial high school), inajengwa kama sehemu ya jitihada za
wilaya hiyo za kumuenzi Sokoine.
Mbali na jitihada za
halmashauri hiyo, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) ambacho pia kimebeba
jina lake kimekuwa katika mikakati ya kuhakikisha kuwa kinamuenzi kiongozi huyo
kwa kila hali.
Kassim Msagati ni ofisa
mawasiliano wa chuo hicho, anasema hayati, Edward Moringe Sokoine, alikuwa
muhimili muhimu wa kuanzishwa wa chuo kikuu hicho cha kilimo ambacho ni chuo
kikuu pekee cha kilimo cha Serikali nchini.
Aprili 12, 1984 bunge la
jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambalo hayati Sokoine alishiriki lilipitisha
sheria namba 6 ya mwaka 1984 ya kuanzishwa kwa chuo kikuu cha kilimo
Morogoro.
Hapo kabla chuo hicho
kilikuwa ni kitivo cha kilimo cha kilimo na misitu cha chuo kikuu cha Dar es
Salaam.
Kwa mujibu wa Msagati, sheria
hiyo iliyopitishwa na bunge ilikiidhinisha kitivo cha kilimo cha chuo kikuu cha
Dar es salaam kilichokuwa Morogoro kuwa chuo kikuu na kutaka kiitwe chuo kikuu
cha kilimo Morogoro.
Lakini chuo hicho
kililazimika kubadilishwa jina hata kabla ya jina la awali kuanza kutumika na
kuitwa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).
Hii ilitokana na kifo cha kiongozi huyo, muda
mfupi baada ya chuo hicho kuidhinishwa rasmi kwa sheria hiyo ambapo utekelezaji
wake ulipaswa kuanza mwezi Julai, 1984, ndipo serikali ikakubali kiitwe Chuo
Kikuu cha Sokoine cha kilimo
Edward Moringe Sokoine alizaliwa
tarehe 1 Agosti 1938 alikuwa Waziri
Mkuu wa Tanzania tarehe 13 Februari
1977 hadi tarehe 7 Novemba
1980 tena akawa Waziri mkuu toka
tarehe 24 February hadi tarehe
12 Aprili 1984. Alikuwa ni mtu
aliyepanda usawa kwa kila mtu aliamini
kila mtu anaweza kuwa na
maendeleo kama akijituma katika kilimo
na sehemu alipo pamoja na
kujitegemea akiwa ni wakala wa
mabadiliko katika nchi, mtu asielaumu
na mwaminifu.
Alizaliwa Monduli Mkoani Arusha
Tanzania, alipata elimu
ya msingi na sekondari katika miji ya
Monduli na Umbwe toka mwaka
1948 hadi 1958. Mwaka 1961
alijiunga na chama cha TANU
baada ya kuchukua masomo katika
Uongozi nchini Ujerumani 1962
hadi mwaka 1963. Aliporudi
kutoka Ujerumani alikuwa Afisa Mtendaji
wa Wilaya ya Masai, tena akachaguliwa
kuwa mwakilishi wa jimbo
la Masai. Mwaka 1967 alikuwa naibu
waziri wa mawasiliano, usafiri
na kazi. Hatua nyingine katika
maisha yake alijitangaza
mpaka kuwa Waziri Mkuu 1970.
Mwaka 1972 aliamia kwenye Waziri wa
usalama. Mwaka 1975
alichaguliwa kwenye Bunge tena wakati
huu kupitia Monduli.
Miaka miwili baadae akawa mjumbe
wa Kamati kuu ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM), 1977 alianza
muhula wa kwanza ofisini akiwa
Waziri Mkuu wa Jamuhuri wa Muungano wa
Tanzania. Muhula huu
ulidumu hadi 1981, baada ya kutulia
kwa kipindi cha mwaka alikuwa
tena Waziri Mkuu tena mwaka 1983,
alikaa mwaka mmoja ofisini
mpaka alipofariki Aprili 1984
kwa ajali ya gari.
Kuna Chuo Morogoro Tanzania kinaitwa jina lake (Sokoine
University Of Agriculture (SUA) kilianza mwaka 1984 kama chuo
cha kilimo kinachotoa diploma katika kilimo. Chuo hicho
kikaongezwa hadi kutoa mchepuo wa
kilimo mwaka 1969 chini ya Chuo
Kikuu Cha Dar Es Salaam.
JINSI AJALI ILIVYOKUWA
Ilikuwa Jumatano ya Aprili
12, 1984 saa 11:30 jioni, siku ambayo Dar es Salaam ilinyesha mvua kutwa
nzima.
Wakati kipindi cha salaam cha
Jioni Njema cha Redio Tanzania (RTD) wakati huo kikiwa hewani, mara matangazo
yake yanakatishwa ghafla na wimbo wa taifa unapigwa.
Mara inasikika sauti
iliyozoeleka ya Rais Nyerere wakati huo ikisema:
“Ndugu wananchi, leo majira
ya saa 10 jioni, ndugu yetu, kijana wetu na mwenzetu, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine wakati akitoka Dodoma kuja Dar es
Salaam, gari yake imepata ajali, amefariki dunia.”
Takribani miaka 30 imepita
tangu kufariki kwa, Edward Moringe Sokoine, aliyepata kuwa waziri mkuu wa
Tanzania katika vipindi viwili tofauti kabla ya kufariki Aprili 12, 1984.
Sokoine alikufa baada ya
kutokea ajali ya gari eneo la Wami-Dakawa, wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro
akiwa njiani kurejea Dar es Salaam akitokea mjini Dodoma alikokuwa akishiriki
vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
KUMBUKUMBU YA
KILA MWAKA:
Aprili 12 ya kila mwaka,
taifa limekuwa likiadhimisha kumbukumbu ya kiongozi huyo kwa kufanya shughuli
mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kuendesha makongamano, midahalo,
mabonanza, ibada, riadha na upandaji mlima Kilimanjaro.
Katika utawala wa hayati baba
wa taifa na rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwalimu Julius
Kambarage Nyerere, katika eneo la Wami Sokoine kulijengwa nyumba moja na
banda moja linalotumika kama jukwaa lakini kwa sasa majengo hayo yamechakaa,
anasema msimamizi wa eneo hilo, Hamis Said Mpandachuri.
Waandishi walifika katika
eneo hilo na kukuta mnara wa picha ya Sokoine ukiwa umepakwa rangi mpya za
manjano, kijani, blue na nyeusi huku chini ya picha yake kukiwa na maneno “Alimtumikia Mungu kwa kuwatumikia watu,
sauti ya watu ni sauti ya Mungu”.
Mbali ya mnara huo na majengo
yaliyojengwa katika utawala wa serikali ya kwanza, pia liko jengo jipya na la
kisasa ambalo linaendelea kujengwa nyuma ya majengo ya zamani.
Kwa mujibu wa uongozi wa
halmashauri ya wilaya ya Mvomero, jengo hilo ni kwa ajili ya shule ya sekondari
ya Sokoine (Sokoine memorial high school), inajengwa kama sehemu ya jitihada za
wilaya hiyo za kumuenzi Sokoine.
Mbali na jitihada za
halmashauri hiyo, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) ambacho pia kimebeba
jina lake kimekuwa katika mikakati ya kuhakikisha kuwa kinamuenzi kiongozi huyo
kwa kila hali.
Kassim Msagati ni ofisa
mawasiliano wa chuo hicho, anasema hayati, Edward Moringe Sokoine, alikuwa
muhimili muhimu wa kuanzishwa wa chuo kikuu hicho cha kilimo ambacho ni chuo
kikuu pekee cha kilimo cha Serikali nchini.
Aprili 12, 1984 bunge la
jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambalo hayati Sokoine alishiriki lilipitisha
sheria namba 6 ya mwaka 1984 ya kuanzishwa kwa chuo kikuu cha kilimo
Morogoro.
Hapo kabla chuo hicho
kilikuwa ni kitivo cha kilimo cha kilimo na misitu cha chuo kikuu cha Dar es
Salaam.
Kwa mujibu wa Msagati, sheria
hiyo iliyopitishwa na bunge ilikiidhinisha kitivo cha kilimo cha chuo kikuu cha
Dar es salaam kilichokuwa Morogoro kuwa chuo kikuu na kutaka kiitwe chuo kikuu
cha kilimo Morogoro.
Lakini chuo hicho
kililazimika kubadilishwa jina hata kabla ya jina la awali kuanza kutumika na
kuitwa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).
Hii ilitokana na kifo cha kiongozi huyo, muda
mfupi baada ya chuo hicho kuidhinishwa rasmi kwa sheria hiyo ambapo utekelezaji
wake ulipaswa kuanza mwezi Julai, 1984, ndipo serikali ikakubali kiitwe Chuo
Kikuu cha Sokoine cha kilimo
No comments:
Post a Comment