Monday, 28 April 2014
BEI YA TANZANITE YAPANDA NCHINI
Na Mussa Juma, Mwananchi
Arusha.Bei ya madini ya Tanzanite yanayopatikana kwenye machimbo ya mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, hapa nchini imepanda huku bei hiyo ikiporomoka katika soko la kimataifa.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwa wafanyabiashara kadhaa wa madini na wachimbaji wa madini hayo, umebaini kupanda kwa bei ya madini hayo hapa nchini, kunatokana na uzalishaji kupungua migodini.
Kwa sasa bei hiyo, imepanda kati ya Sh100,000 hadi Sh500,000 kwa gramu moja ya Tanzanite kutokana na ubora na ukubwa.
Hata hivyo, katika soko la kimataifa, bei hiyo imeporomoka kutokana na madini hayo kusafirishwa nje kwa wingi zaidi miaka ya karibuni.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Maruti Green Gems Limited, Faisal Juma Shahbhai, alisema bei ya madini haya imekuwa ikipanda hapa nchini kutokana na uzalishaji kupungua.
Hata hivyo, alisema hali ya utulivu na amani, katika migodi ya Tanzanite pia imechangia kuimarika kwa biashara ya madini hayo hapa nchini.
Mwenyekiti wa Chama cha Wauzaji wa madini nchini (Tamida), Sammy Mollel alisema kwa sasa uzalishaji wa madini hayo umekuwa mdogo, kutokana na gharama kubwa na uchimbaji.
MWISHO.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
hello habari naomba taarifa za gharama kwa madini ya amethyst pamoja na red gunet number angu +255712275701
ReplyDelete