Mradi huo wa barabara
uliokabidhiwa serikali Mei 31 mwaka huu, mkandarasi wake anaendelea na kazi
ndogo ndogo za ujenzi wa mifereji ya maji ya mvua, vivuko na vituo vya basi
hasa eneo la Kairo.
Meneja wa wakala wa
barabara nchini (Tanroads) mkoa wa Manyara, mhandisi Bashiri Rwesingisa
aliyasema hayo wakati akisoma taarifa ya mradi huo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Ujenzi) mhandisi Joseph Nyamhanga
alipotembelea eneo hilo.
Mhandisi Rwesingisa
alisema barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 27 iliyojengwa na kampuni ya
China Henan International Cooperation Group (Chico) kwa gharama ya sh32.2
milioni, chini ya usimamizi wa ujenzi mhandisi mshauri M/s LEA International
Ltd ya India kwa ushirikiano na kampuni ya DOCH Tanzania Ltd.
Alisema kazi
zilizotekelezwa ni ujenzi wa kiwango cha lami urefu wa kilometa 27 ikijumuisha
Kia hadi Mirerani, Mirerani hadi eneo la uwekezaji la (EPZ), barabara ielekeayo
Arusha inayopitia Mbuguni, barabara ya kuingia na kutoka kituo cha mabasi
Mirerani na mzunguko kiwanda cha TanzaniteOne.
"Ujenzi wa barabara
hii umehusisha pia kujenga mifereji ya pembezoni mwa barabara kwenye maeneo ya
mji, sehemu za kuvuka mifugo na sehemu za kuvushia huduma muhimu kama waya za
simu na umeme," alisema mhandisi Rwesingisa.
Alisema mradi huo
umekuwa na changamoto za migomo ya wafanyakazi, wananchi kugoma kuondoa mali
zao ndani ya hifadhi ya barabara.
Alisema mipango ya
baadaye ni kujenga kilometa 114 barabara kwa kiwango cha lami itakayounganisha
eneo la EPZ na mji mdogo wa Orkesumet, makao makuu ya wilaya ya Simanjiro, kama
ilivyoainishwa kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015.
Akizungumza baada ya
kukagua mradi huo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulikia ujenzi, mhandisi
Joseph Nyamhanga alipongeza jitihada zilizofanyika kwa pande zote hadi barabara
hiyo ikamalizika.
Mhandisi Nyamhanga
alisema wakati wanasubiri barabara hiyo kuzinduliwa wakati inaendelea kutumika,
watumiaji wanapaswa kufuata masharti ya matumizi ya barabara hiyo ili
waitunze.
Aliitaka jamii ya eneo
hilo ambao kwa muda mrefu walikuwa wanalilia utengenezwaji wa barabara na ndiyo
wanufaika wa mradi huo, kuutunza vizuri kwani ni kwa ajili ya faida yao na
vizazi vijavyo.
No comments:
Post a Comment