Saturday 6 October 2012

HARAMBEEE

MKUU wa Mkoa wa Manyara,Elaston Mbwilo ameongoza harambe na kupatikana shilingi 5,050,000 (milioni tano na elfu hamsini) kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za kuishi askari wa kituo cha polisi cha kata ya Naisinyai wilayani Simanjiro.

Mbwilo ambaye alichangia shilingi milioni moja alianzisha harambee hiyo jana ili nyumba hizo za askari wa kituo hicho kipya cha Polisi kata ya Naisinyai zijengwe na waweze kuishi kwani zitawapunguzia askari hao kero ya makazi.

Aliagiza wananchi,viongozi wa kijij na kata ya Naisinyai wakishirikiana na kampuni ya TanzaniteOne kuhakikisha kuwa wanamaliza ujenzi wa nyumba hizo kabla ya mwezi Desemba ili aweze kuzindua rami kituo hicho.

“Nikizindua leo kituo hiki bila kuwa na nyumba za kuishi askari wetu hata ninyi mtanishitaki hivyo nawachangia sh milioni moja na muongeze nguvu mkishirikana na TanzaniteOne ili mjenge nyumba hizo nije nizindue,” alisema Mbwilo.


No comments:

Post a Comment