Baadhi
ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Manyara, wakiwa kwenye kikao jana mjini
Babati na ujumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ukiongozwa na Makamu Mwenyekiti
wa Tume hiyo, Jaji Mkuu mstaafu wa Zanzibar, Hamid Mahamoud Hamid, ambapo walipatiwa elimu ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia
mfumo wa teknolojia mpya ya Biometric Voter Registration (BVR) unatarajia
kuanza mwezi Septemba mwaka huu.
.Monday, 30 June 2014
TUNAANGALIA BONANZA LA WAANDISHI ARUSH
Mgeni Rasmi katika Bonanza la Vyombo vya Habari mkoani
Arusha, Juma Pinto wa pili kushoto, akifuatilia michezo iliyokua inaendelea kwenye
uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha wengine kushoto ni Le
Mutuz, Mkurugenzi wa Mireranitanzanite.blogspot, Joseph Lyimo na Meneja Uhusiano wa Kampuni
ya Mega Trade, Goodluck Kway.
Sunday, 29 June 2014
NACHANGIA DAMU
Mkazi wa Mji
mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoniani Manyara, Japhary Matimbwa
akichangia damu kwenye kituo cha Afya Mirerani, ambapo katika zoezi la
kuchangia damu lita tatu pekee zilipatikana baada ya watu watatu kujitokeza
kuchangia damu (kushoto) ni mtaalamu wa maabara wa kituo hicho, Dr Fanuel
Laizer.
Friday, 27 June 2014
MADEREVA WA BODABODA WALIPOGOMA
Askari Polisi Jamii wa Tarafa ya Moipo Wilayani Simanjiro Mkoani
Manyara, AS/INSP Amiri Mlemba, akizungumza na madereva wa pikipiki za kubeba
abiria ambao waliandamana hadi kwenye kituo cha polisi Mirerani wakipinga kutozwa fedha na
maofisa biashara wa wilaya hiyo.
Mkuu wa kituo cha polisi Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani
Manyara, ASP Lwitiko Kibanda, akizungumza na madereva wa pikipiki za kubeba
abiria ambao waliandamana hadi kwenye kituo hicho wakipinga kutozwa fedha na
maofisa biashara wa wilaya hiyo.
Mkuu wa kituo cha polisi Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani
Manyara, ASP Lwitiko Kibanda, akizungumza na madereva wa pikipiki za kubeba
abiria ambao waliandamana hadi kwenye kituo hicho wakipinga kutozwa fedha na
maofisa biashara wa wilaya hiyo.
Subscribe to:
Posts (Atom)