Tuesday, 30 December 2014
NAKUUZIA MADINI YA TANZANITE
Mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Gerald Biko (kulia) akimuuzia Daudi Luambe madini hayo, Tanzanite ni madini ambayo hupatikana Mirerani pekee hapa duniani.
Friday, 26 December 2014
TUNAKULA KIAPO
Wenyeviti wa Vitongoji vya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakiapishwa na Hakimu Godfrey Haule wa Mahakama ya Mwanzo Mirerani.
Hakimu Godfrey Haule wa Mahakama ya Mwanzo Mirerani, akiwapa somo Wenyeviti wa Vijiji, Vitongoji na wajumbe wa Serikali za Mitaa wa Tarafa ya Moipo kabla ya kuwaapisha.
Wenyeviti wa Vitongoji vya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakiapishwa na Hakimu Godfrey Haule wa Mahakama ya Mwanzo Mirerani.
MAREMA WAOMBA HISA
Mussa Juma Mwananchi
Arusha. Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini cha Manyara (Marema) kimeitaka Serikali kukipa asilimia 50 ya hisa zake katika migodi ya TanzaniteOne iliyopo Mirerani na kuipongeza kampuni ya wazawa ya Sky Associates Group (LTD) kwa kununua asilimia nyingine 50 ya hisa.
Mwenyekiti wa Marema, Sadiki Mnenei alisema ofisini kwake juzi kuwa kampuni hiyo ya wazawa ambayo imenunua hisa kwa Sh32 bilioni, imeonyesha jinsi wazawa walivyo na uwezo wa kuwekeza wakipewa nafasi na kuondoa dhana kuwa hawana uwezo.
“Sisi tunawapongeza wenzetu kwa kununua asilimia 50 ya hisa zilizokuwa zinamilikiwa na kampuni ya Richland Resources ya England ndani ya TanzaniteOne katika migodi ya kitalu C ya machimbo ya Tanzanite na tunataka tupewe hisa zilizobaki,” alisema.
Alisema sheria ya madini ya vito, inaeleza wazi madini hayo yatachimbwa na wazawa, umefika wakati kwa Serikali kuachia asilimia 50 ya hisa hizo kwa wazawa badala ya kuzipeleka kwa shirika la Stamico ambalo alidai kuwa lina majukumu mengi.
“Wanachama wetu wana uwezo, tupewe asilimia 50 na tupo tayari kuzinunua ili kilio cha miaka mingi cha wachimbaji wadogo kiwe kimepatiwa ufumbuzi,” alisema.
Mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya Sky associated Group Ltd, Faisal Shahbhai alisema wako tayari kufanya kazi na wadau wote wa madini ya tanzanite katika kuhakikisha Watanzania wananufaika na madini hayo.
“Sisi tunaomba ushirikiano na wadau wote wa madini ili tuweze kuongeza uzalishaji wa madini haya pia kuibua masoko mapya ya uhakika ndani na nje ya nchi,” alisema.
Kampuni ya TanzaniteOne ilikuwa inamiliki leseni ya uchimbaji madini (SML 8/92) kwa asilimia 100 kabla ya Serikali kuingia ubia kupitia Stamico ambayo bado inamiliki asilimia 50 ya hisa kutokana na kutekeleza matakwa ya kisheria ya uchimbwaji wa madini ya vito.
Thursday, 25 December 2014
MWENYEKITI WETUUU
Wananchi wa Kijiji
cha Kambi ya Chokaa, Kata ya Naisinyai Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara,
wakiwa wamembeba juu Joshua Kuney ambaye alishinda kwenye kura ya maoni ya CCM
kuwa Mwenyekiti wa kijiji hicho kwa kura 335 dhidi ya Mbuki Mollel aliyepata
kura 215.
Wednesday, 24 December 2014
MWENYEKITI AKATALIWA KUHAPISHWA
Mwenyekiti mteule wa
Kijiji cha Kambi ya Chokaa, Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Mbuki Mollel
akiwa kwenye Mahakama ya mwanzo Mirerani, ambapo Hakimu Godfrey Haule aligoma
kumuapisha akidai kuwa kuna utata wa uteuzi wake kwani anadaiwa kushindwa na
Joshua Kuney kwenye uchaguzi wao.
Subscribe to:
Posts (Atom)