Monday, 13 January 2014

RIP FORTUNATHA RINGOBaadhi ya watu waliohudhuria mazishi ya mwaandishi wa habari wa gazeti la Habari Leo Mkoani Manyara, marehemu Fortunatha Ringo aliyefariki dunia Januari 10 mwaka huu jijini Dar es salaam kwa ugonjwa wa kuishiwa damu na kuzikwa Januari 13 kwenye kijiji cha Mdawi Old Moshi.

Tukiwa na Meneja wa Radio Safina Arusha Jovin Msuya tukiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Fortunatha Ringo, mwandishi wa habari wa gazeti la Habari Leo Mkoani Manyara aliyefariki Januari 10 jijin Dar es salaam na kuzikwa Januari 13 kijijini Mdawi Old Moshi.

Wilfred Ringo na Doktael Ringo, wazazi wa mwandishi wa gazeti la Habari Leo Mkoani Manyara, marehemu Fortunatha Ringo, wakiuaga mwili wa mtoto wao aliyefariki jijini Dar es salaam Januari 10 mwaka huu na kuzikwa kijijini Mdawi Old Moshi, Januari 13 mwaka huu.


Jeneza lenye mwili wa mwandishi wa habari wa gazeti la Habari Leo Mkoani Manyara, marehemu Fortunatha Ringo aliyefariki dunia Januari 10 mwaka huu jijini Dar es salaam kwa ugonjwa wa kuishiwa damu ujulikanao kitaalam kama Auto Immune Disease baada ya dawa za malera kumdhuru mwaka 2011, likiingizwa kaburini na kuzikwa Januari 13 kwenye kijiji cha Mdawi Old Moshi.


Baadhi ya waandishi wa habari wa mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro, wakibeba jeneza lenye mwili wa mwandishi wa habari wa gazeti la Habari Leo Mkoani Manyara, marehemu Fortunatha Ringo aliyefariki dunia Januari 10 mwaka huu jijini Dar es salaam kwa ugonjwa wa kuishiwa damu na kuzikwa Januari 13 kwenye kijiji cha Mdawi Old Moshi.

No comments:

Post a Comment