Akizungumza
wakati akitoa tamko lake la kujitoa NCCR Mageuzi na kujiunga na Chadema,Tara
alisema amejitoa kwenye chama hicho akiwa na sababu kuu mbili zilizosababisha
yeye kuhama chama hicho.
Alizitaja
sababu hizo kuwa ni baadhi ya viongozi wa NCCR Mageuzi kupendelea au kuendeleza
urafiki na mfumo dhalimu wa dhuluma na maovu yanayofanywa na dola chini ya
Serikali ya CCM.
Alisema
kutokana na hali halisi ya kisiasa nchini ilipofika na kwa jinsi dhuluma na
maovu kushamiri nchini kiasi cha kufikia watumishi na viongozi wa umma
kudhulumu na kufanya maovu kwa uhuru mkubwa bila hofu ya kuadhibiwa.
“Tunahitajika
chama cha siasa,kilicho makini na ambacho watanzania tunapaswa kuunganisha
nguvu zetu kwa pamoja bila kutengana na kwa maoni yangu NCCR Mageuzi siyo chama
cha aina hiyo,” alisema Tara.
|
No comments:
Post a Comment