Naibu
Katibu Mkuu wa chama cha NCCR-Mageuzi (Bara) Lawrence Surumbu Tara ambaye pia
ni Diwani wa kata ya Bashnet Wilayani Babati Mkoani Manyara (katikati)
akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Babati ambapo alitangaza rasmi
kujivua udiwani na vyeo vyote alivyokuwa navyo NCCR-Mageuzi na kujiunga na
Chadema (kushoto) ni aliyekuwa mbunge wa Arusha Godbess Lema na,Kamanda Ally
Bananga.
Alisema
yeye ni mmoja wa waathirika wa mfumo huo mbovu wenye dhuluma kwani alidhulumiwa
ubunge kwenye uchaguzi wa mwaka 2010 na kwa bahati mbaya wizi huo wa kura
unaongeza maovu.
Alisema
yeye alishinda ubunge wa Jimbo la Babati Vijijini kwa kupata kura kura 32,248
na mgombea wa CCM akapata kura 30,190 lakini baadhi ya wasimamizi v
wakabadilisha matokeo na kumpa mgombea wa CCM kura 32,777 na yeye 31,635.
“Kule
Dareda niliibiwa kura 156 na shule ya msingi Riroda niliibiwa kura 300 na Chadema
wakaibiwa kura 10 ambazo zilijumlishwa kwa CCM na akaongezea kura hewa 48
kwenye shule ya msingi Riroda namba 4 na Mwada shule ya msingi shauri moyo CCM
walipewa kura hewa 400.
Alisema
katika mazingira hayo amebakiwa na chaguo moja wapo kati ya kubaki ndani ya
chama kisichokerwa na wizi wa kura na ambao baadhi ya viongozi wake
wanaendeleza urafiki na mfumo huo uliokithiri.
“Nikaona
kujitenga na kuachana na chama chenye viongozi wa aina hiyo na kutafuta chama
imara ambacho hakina simile na mambo kama ya aina hio chenye kupigania
haki,ukweli na ambacho kimepania utawala bora na ustawi wa watanzania,”
alisema.
na,Kamanda Ally
Bananga.
|
No comments:
Post a Comment