Dc Mbulu aanzisha kampeni ya vyeti
vya kuzaliwa, vifo na ndoa kwa manufa ya wananchi.
Mkuu wa wilaya ya Mbulu Mkoani
Manyara Chelestino Simbalimile Mofuga ameanzisha kampeni ya wananchi wilayani Mbulu ya vyeti vya kuzaliwa, vifo na ndoa.
kampeni hiyo imezinduliwa katika kata
tatu ikiwemo kata ya Ayamaami, Uhuru na kata ya Imboru.
Mofuga amesema ni vyema kila mwananchi
kuwa na cheti cha kuzaliwa ili kuepuka usumbufu na kutambulika katika eneo
lake kwani mwananchi akiwa na cheti cha
kuzaliwa anakuwa salama na akihitaji huduma ni rahisi kuhudumiwa katika eneo
lake.
pamoja na hilo amesema vyeti vya ndoa
na vifo ni muhimu sana kwa mwananchi ili inapotokea mmoja amefariki itamsaidia
ailiyebaki katika kusimamia mirathi bila kuingiliwa na mtu yeyote wa upande
mwingine.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya Mbulu
amesema kwamba wilaya ya Mbulu inakabiliwa na
changamoto ya matumizi ya risiti na kuwataka wananchi kutoanunua bidhaa
katika maduka ambayo hayatoi risiti ili kuepuka usumbufu wa kupelekwa kwenye
vyombo vya sheria kwani mwananchi akikamatwa ana bidhaa aliyonunua bila risiti
atafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
katika maeneo hayo aliyoyapitia
nakufanya mkutano wa hadhara mkuu wa wilaya amewataka wananchi kutopika wala
kunywa pombe haramu aina ya gongo na pia kutouza pombe kabla ya saa tisa alasiri.
Kwa kata ya Uhuru ameagiza wenyeviti
wa mitaa kusimamia wananchi wasinywe pombe kabla ya saa tisa vinginevyo watawajibika
wao wenyewe kwani mtaa wa Uhuru unasifika sana kwa unywaji wa pombe badala ya
kufanya kazi.
Katika kata tatu alizoanza nazo
tarehe 8.06.2018 katika kata tatu ambazo ni kata ya Ayamaami,uhuru na Imboru
kata ya Imboru mahudhurio hayakuwa mazuri na ameagiza wenyeviti wa mitaa
siku ya tarehe 11.06.2018 kufika katika
ofisi yake wakiwa na maelezo ya kutosha ya kwanini wananchi hawajajitokeza.
Pamoja na maelezo hayo amewataka
wenyeviti waende na tozo ya shilingi 5,000/ kwa kila kichwa kwa wale wote ambao hawahudhuria kikao chake cha kiserikali
yenye lengo la kutoa maagizo muhimu.
Amesema wananchi wote ambao
hawajashiriki mkutano wake wanafikia 1004
na kwa tozo hizo watakazotoa watafikisha million tano ambayo imepitishwa
kupelekwa kwenye shule ya msingi Isale kwa ajili ya kupeleka maji.
Kauli mbiu cheti cha kuzaliwa nyumba
kwa nyumba
No comments:
Post a Comment