Nyongo aliyasema hayo alipotembelea mji mdogo
wa Mirerani wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa ukuta na eneo litakalofanyika mnada
wa madini ya Tanzanite.
Alisema shughuli za ujenzi wa ukuta ni za
kujitolea siyo za biashara ya kupata faida hivyo wafanyabiashara wasitake
faida.
Alisema wafanyabiashara wanapaswa kutumia
fursa ya ujenzi wa ukuta huo kwa kufanya biashara na kupata faida kidogo kuliko
kuweka tamaa ya kuuza vitu bei ghali.
"Rais John Magufuli wakati anazindua
barabara ya lami ya Kia-Mirerani Septemba 20 mwaka huu alitoa agizo la kujengwa
kwa ukuta kwa lengo la kulinda rasilimali hii adimu hivyo wafanyabiashara
wasijinufaishe," alisema Nyongo.
Aliwapongeza askari wa jeshi la kujenga Taifa
kupitia shirika la Suma JKT kwa namna wanavyofanya shughuli hiyo ya kujenga
ukuta kutokana na kasi iliyopo.
Alisema ana imani kazi hiyo itachukua muda wa
miezi sita kama Rais Magufuli alivyoagiza na wao kama wizara wataendelea kutoa
ushirikiano kwa jeshi hilo.
Awali, mkuu wa wilaya ya Simanjiro mhandisi
Zephania Chaula alisema askari hao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali
ikiwemo ya magari yanayobeba vifaa vya ujenzi kusimamishwa na askari polisi wa
usalama barabarani wa mkoa wa Arusha, hivyo kuwachelewesha kwenye ujenzi.
Mhandisi Chaula alisema ili kuhakikisha hilo
alifanyiki tena wameamua kuweka karatasi maalumu kwenye magari yanayobeba vifaa
vya ujenzi wa ukuta huo ili wasisumbuliwe tena.
Alisema walitoa taarifa ngazi ya mkoa wa
Manyara ili wakutane na mkoa wa Arusha, kwa lengo la kuzungumza na kumaliza
changamoto za ujenzi huo.
No comments:
Post a Comment