Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani
Manyara, Hudson Starnley Kamoga (kushoto) akikagua mabomba ya maji kwenye mradi wa
Kijiji cha Endamasak, kulia ni mhandisi wa maji wa Halmashauri hiyo John Michael.
Wednesday, 22 November 2017
DED KAMOGA AKIITUMIKIA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBULU
NAIBU WAZIRI WA MADINI LADSLAUS NYONGO AWATAKA WAUZA VIFAA VYA UJENZI WA UKUTA KUTOPANDISHA VIFAA BEI
Naibu Waziri wa Madini
Ladslaus Nyongo amewataka wauzaji wa vifaa vya ujenzi wa ukuta unaozunguka
migodi ya madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro
Mkoani Manyara, kutowauzia wanajeshi bei ghali vifaa vinavyojengea ukuta
huo.
Nyongo aliyasema hayo alipotembelea mji mdogo
wa Mirerani wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa ukuta na eneo litakalofanyika mnada
wa madini ya Tanzanite.
Alisema shughuli za ujenzi wa ukuta ni za
kujitolea siyo za biashara ya kupata faida hivyo wafanyabiashara wasitake
faida.
Alisema wafanyabiashara wanapaswa kutumia
fursa ya ujenzi wa ukuta huo kwa kufanya biashara na kupata faida kidogo kuliko
kuweka tamaa ya kuuza vitu bei ghali.
"Rais John Magufuli wakati anazindua
barabara ya lami ya Kia-Mirerani Septemba 20 mwaka huu alitoa agizo la kujengwa
kwa ukuta kwa lengo la kulinda rasilimali hii adimu hivyo wafanyabiashara
wasijinufaishe," alisema Nyongo.
Aliwapongeza askari wa jeshi la kujenga Taifa
kupitia shirika la Suma JKT kwa namna wanavyofanya shughuli hiyo ya kujenga
ukuta kutokana na kasi iliyopo.
Alisema ana imani kazi hiyo itachukua muda wa
miezi sita kama Rais Magufuli alivyoagiza na wao kama wizara wataendelea kutoa
ushirikiano kwa jeshi hilo.
Awali, mkuu wa wilaya ya Simanjiro mhandisi
Zephania Chaula alisema askari hao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali
ikiwemo ya magari yanayobeba vifaa vya ujenzi kusimamishwa na askari polisi wa
usalama barabarani wa mkoa wa Arusha, hivyo kuwachelewesha kwenye ujenzi.
Mhandisi Chaula alisema ili kuhakikisha hilo
alifanyiki tena wameamua kuweka karatasi maalumu kwenye magari yanayobeba vifaa
vya ujenzi wa ukuta huo ili wasisumbuliwe tena.
Alisema walitoa taarifa ngazi ya mkoa wa
Manyara ili wakutane na mkoa wa Arusha, kwa lengo la kuzungumza na kumaliza
changamoto za ujenzi huo.
MACHIMBO YA DHAHABU NYARUGUSU
Mchimbaji wa madini ya dhahabu kwenye machimbo
ya Nyarugusu Mkoani Geita, Christopher Kadeo akizungumza na wadau wa madini
waliotembelea mgodi wake.
LOWASSA AMNADI MGOMBEA UDIWANI MAKIBA NA KUKANUSHA KUTAKA KWENDA CCM
Waziri Mkuu mstaafu na mjumbe wa Baraza Kuu la
Chadema, Edward Lowassa, amemshukia Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kuwa
asitafute umaarufu wa kisiasa kwa kutumia jina lake.
Akizungumza jana kwenye mkutano wa kampeni ya
kumnadi Joyce Rutha (Chadema) mgombea udiwani wa kata ya Makiba Wilayani
Arumeru Mkoani Arusha, Lowassa alisema hujatuma watu kwa Gambo ili arudi
CCM.
Alisema kuendelea kumzungumzia Gambo kwenye majukwa ya kisiasa ni kumpa umaarufu wa bure kwani yeye hujamtuma mtu au watu kutoka Monduli ili aende kwa mkuu huyo wa mkoa kwa lengo la kuomba arudi CCM.
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo jana
kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii ya Facebook, Instagram na tweeter,
aliandika kuwa amepokea ujumbe kutoka Monduli.
Gambo aliandika kuwa ujumbe huo ulikuwa na
ombi moja kubwa amuombee mzee wa Monduli kwa Rais Magufuli ili akubali kumuona
na yeye yupo tayari kurudi nyumbani kama Rais atakubali kumuona.
Alisema ujumbe huo unasema ombi hilo katuma
muda mrefu bila majibu.
"Mnao mfahamu mzee huyu mfikishieni
ujumbe kuwa salamu nitaifikisha, mjumbe hauwawi," aliandika Gambo.
Lowassa alisema jana mchana alisoma kwenye
mitandao ya kijamii kuwa ametuma watu wamuombee ili arudi CCM jambo ambalo siyo
kweli.
"Siwezi kumjibu huyu kijana kwani
kuendelea kumjadili ni kumpa umaarufu hivyo simjibu chochote kwenye hilo,"
alisema Lowassa.
Akizungumza wakati wa kumnadi mgombea udiwani
huyo, Lowassa aliwataka wananchi wa kata ya Makiba kumpa kura nyingi za ndiyo
Rutha ili awe diwani wao.
"Mwaka 2015 nilikuja kuwaomba kura na
mkanipa kwa wingi sasa endeleeni kuikataa CCM kwa kumpa kura mgombea wetu wa
Chadema Rutho," alisema Lowassa.
Pia, alisema wananchi zaidi ya milioni sita
waliompigia kura nao wanapaswa kusemewa na wao kwa kuwepo kwa serikali ya
mseto.
Alisema katiba mpya ni jibu kwa kuweka
kipengele cha serikali ya mseto kwa mlengo wa kushoto na kulia ili mtu mmoja
asipate nafasi ya kuharibu vitu vingi.
Alisema hata Marekani na Ufaransa
wanashirikiana kwenye nafasi hizo pindi uchaguzi ukifanyika bila kujali chama
ni cha kijamaa au kibepari.
"Japo kuna wabunge lakini wale watu
milioni sita walionipigia kura nao wanapaswa kuwakilishwa serikali kama wale
milioni nane wengine ambao wana mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya,
wakurugenzi na viongozi wengine," alisema Lowassa.
Nassari alisema wananchi wanapaswa kumchagua
Rutha bila kujali kabila lake kwani jambo la muhimu ni kusimamia
maendeleo.
Alisema Rutha ni mgombea mwadilifu kwani
wapinzani wao waliweza kumrubuni kwa sh5 milioni na kumwekea pingamizi lakini
tume ikamrudisha.
Ole Millya alisema anashangazwa na watu
waliokuwa Chadema kisha wanarudi CCM ili hali hakuna jambo kubwa walilofanyiwa
hadi kusababisha kuachana na chama hicho zaidi ya tamaa.
"Ni kwa furaha gani wewe Mollel unarudi
CCM, ili hali wafugaji wanaendelea kuteseka kote Tanzania, jibu la yote hayo ni
kuendelea kuwa Chadema na siyo kukimbia," alisema Ole Millya.
Mgombea udiwani wa kata hiyo Joyce Rutha
alisema endapo atachaguliwa kuwa diwani, atahakikisha anakuwa mwakilishi mwema
wa wananchi wa eneo hilo kwenye halmashauri ya wilaya hiyo.
Rutha alisema ataendelea kufanya kampeni ya
nyumba kwa nyumba ili ahakikishe Chadema inashinda kwenye nafasi hiyo.
WAANDISHI WA HABARI WA MANYARA NA ARUSHA
Waandishi
wa habari wa Mikoa ya Manyara na Arusha wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu
wa Wilaya ya Mbulu Chelestino Mofuga baada ya kupata mafunzo ya namna ya
kuandika maombi ya ruzuku kwa Tanzania Media Foundation (TMF) Mjini Babati.
Friday, 10 November 2017
RC MNYETI ATEMBELEA UKUTA MIRERANI
Mkuu wa Mkoa wa
Manyara Alexander Mnyeti, ameanza rasmi kazi Mkoani humo kwa kukagua ujenzi wa
ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani
Simanjiro, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli.
Alitoa shukrani kwa serikali ya wilaya ya Simanjiro kwa ushirikiano mkubwa
wanaowapa askari hao wakati wa utekelezaji wa ujenzi wa ukuta huo.
Mnyeti alitembelea eneo hilo na mwenyeji wake
mkuu wa wilaya hiyo mhandisi Zephania Chaula na kamati ya ulinzi na usalama ya
mkoa huo.
Alipongeza kasi ya maandalizi ya ujenzi huo
kwani kila sehemu aliyokagua ambapo ukuta utapita aliwakuta vijana hao wa JKT
wana ari na hamasa ya utendaji kazi.
"Kwa namna vijana wetu wanajeshi
wanavyoonekana kwenye maeneo yote niliyopitia wanaonyesha wataimaliza kazi hii
ndani ya muda mfupi tofauti na agizo la miezi sita lililotolewa na Rais
Magufuli," alisema Mnyeti.
Aliwaahidi kutoa ushirikiano kwa jambo lolote
lile watakalokuwa wanalitaka kwenye serikali ili kuhakikisha agizo hilo la Rais
Magufuli linatekelezeka kwa wakati husika.
Kamanda wa operesheni ukuta Mirerani, Kanali
Festus Mang'wela alimhakikishia mkuu huyo wa mkoa kuwa vijana wote wanaojenga
ukuta huo watafikishiwa ujumbe wa kujikinga na maambukizi ya VVU kwa lengo la
manufaa ya kulinda afya zao.
Kanali Mang'wela alisema ukuta huo wenye
kilometa 24.5 na urefu wa mita tatu kwenda juu umeanza kujengwa rasmi Novemba 6
mwaka huu.
Alisema mkuu wa JKT Meja jenerali Michael
Isamuhyo ndiye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo wa ukuta wanaotarajia
kuujenga kwa muda usiopungua miezi sita.
Katibu Tawala wa wilaya ya Simanjiro, Zuwena
Omary akisoma taarifa ya Wilaya hiyo kwa mkuu wa mkoa huo alisema
wanashirikiana ipasavyo katika maandalizi ya ujenzi wa ukuta huo.
Alisema serikali ya wilaya ya Simanjiro na
uongozi wa JWTZ wamekuwa na mawasiliano ya mara kwa mara ili kuhakikisha zoezi
hilo linafanyika ipasavyo na kwa wakati muafaka.
Alisema ukuta huo utachangia kudhibiti
utoroshwaji wa madini hayo ambayo huuzwa yakiwa ghafi au kusanifiwa na kuuzwa
na madalali na wanunuzi wa ndani na nje ya nchi.
Alisema katika utekelezaji wa agizo la Rais
Magufuli, wamefanikisha uanzishwaji wa ujenzi wa ukuta na kupatikana eneo la
mnada wa madini ya Tanzanite Mirerani.
"Hadi hivi sasa imeshafanyika minada
minne ya madini ya Tanzanite jijini Arusha na serikali kuu na halmashauri ya
wilaya ya Simanjiro zikapata kodi ya mapato na kodi ya huduma ila minada ijayo
itafanyika Mirerani," alisema Omary.
WACHIMBAJI WAKUTANA GEITA KUMNYANYUA ZAIDI MCHIMBAJI MDOGO
Mkuu wa Mkoa wa Geita Robert Luhumbi amewataka
wadau wa madini kuhakikisha sekta hiyo inaakisi maendeleo ya jamii inayozunguka
eneo hilo ili waone faida ya kuwepo kwa rasilimali hiyo muhimu.
Akizungumza kabla ya washiriki hao hawajaanza safari ya kutembelea
migodi ya madini ya dhahabu, Luhumbi alisema faida ya uwepo.
Alisema uwepo wa rasilimali ya madini ya
dhahabu mkoani Geita bado haujaonekana ipasavyo kwa jamii ya eneo hilo kwani
zinapaswa kuboresha miundombinu mbalimbali ikiwemo ya barabara, maji, elimu,
afya na mengineyo.
Alisema sekta ya wachimbaji wadogo wa madini
inafanywa na idadi ya watu milioni moja hadi milioni moja na nusu nchini hivyo
wanapaswa kuwekewa mazingira rafiki yatakayoboeesha maisha yao.
Mkurugenzi wa asasi ya Haki Madini, Amani
Mhinda alisema wameandaa mdahalo huo kwa uwezeshwaji wa taasisi ya kimataifa ya
mazingira (IIED) kituo cha kimataifa cha utafiti wa misitu (CIFOR) na kampuni
ya ushauri ya MTL.
Mchimbaji wa madini wa kampuni ya Nsangano
Gold mine, Renatus Nsangano alisema bado wachimbaji wadogo wana changamoto ya
kufanya kazi bila kufanya utafiti.
Luhumbi aliyasema hayo mjini Geita kwenye
ufunguzi wa majadiliano ya wachimbaji wadogo Tanzania yaliyowashirikisha wadau
wa madini wa nchi mbalimbali duniani.
"Hatutaki kuona rasilimali ya madini
inaoneka kuwa ni laana kwa jamii badala ya baraka, kwani kupitia tunu hiyo
wananchi wanapaswa kunufaika kwa kuona maendeleo yanafanywa kwenye maeneo
hayo," alisema Luhumbi.
Mhinda alisema lengo ni kutoa suluhu juu ya
changamoto zinazomkumba mchimbaji mdogo nchini na kupendekeza majawabu.
Alisema sekta ya uchimbaji madini nchini ni
kati ya sekta zinazokua kwa kasi kubwa na yenye mchango mkubwa wa uchumi wa
Taifa.
Alisema ingawa mipango mahususi ya kisera juu
ya uchimbaji mdogo imeanzishwa, bado kuna changamoto nyingi hasa katika uelewa,
ujasiri, mipango, fedha na taratibu zinazokwamisha utekelezaji wa sera na
maboresho.
Nsangano alisema endapo wangekuwa wanafanya
utafiti na kubaini madini yalipo ingekuwa na tija kubwa kwa wachimbaji
wengi.
Hata hivyo, alisema wamesaidia jamii
zinazowazunguka kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya elimu, afya na maji.
Subscribe to:
Posts (Atom)