Nikiwa kwenye utalii wa ndani
Hifadhi ya Taifa ya Tarangire Tarangire
ilianzishwa Juni 19 mwaka 1970 kupitia tangazo la Serikali namba 160 likiwa na
eneo la kilomita za mraba 2,850 na asilimia nane ya mfumo wa ikolojia wa
Tarangire-Manyara wenye kilomita 35,000.
Mkuu wa Hifadhi
ya Tarangire Stephano Qolli anasema hifadhi hiyo ilianzishwa ili kuhifadhi
maeneo ya mto Tarangire na ardhi oevu ambayo ni chanzo pekee cha maji katika
kipindi cha kiangazi, kwani kipindi hicho kinakuwa na mkusanyiko mkubwa wa
wanyama kwenye eneo hla hifadhi.
Qolli anaeleza
kuwa vivutio vilivyopo kwenye hifadhi hiyo ni idadi kubwa ya wanyama wa aina
mbalimbali ikiwemo Tembo (nyumbani kwa tembo), mto Tarangire, Uhamaji wa
wanyama kwa makundi makubwa wakiwemo nyumbu na pundamili, ardhi owevu za silale
na Lamakau, ndege wa aina mbalimbali ambazo ni zaidi ya aina 550 na miti
mikubwa ya mibuyu.
Kwa upande wake,
Mkuu wa idara ya utalii, Beatrice Kessy anasema bidhaa za utalii zilizopo Tarangire
ni utalii wa kuona wanyama kwa gari mchana, utalii wa kuona wanyama usiku,
utalii wa kutembea kwa miguu, utalii wa kuruka na puto, utalii wa kupiga picha
na filamu, utalii wa kupiga kambi ndani ya hifadhi na utalii wa kula chakula
cha moto porini.
No comments:
Post a Comment