Jamii ya wafugaji wa kidatoga wa bonde la
Yaeda Chini Wilayani Mbulu Mkoani Manyara, wakiwasikiliza baadhi ya viongozi wa
wilaya hiyo waliowatembelea ili kusuluhisha mgogoro wao wa ardhi na jamii ya
wairaqw.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara,
Christina Mndeme ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Hanang’ akizungumza na jamii
ya wafugaji wa kidatoga na wairaqw wa Bonde la Yaeda Chini, ambao wana mgogoro
wa muda mrefu,ambapo aliwataka wadumishe amani kwenye eneo hilo.
Mkuu wa polisi wa Wilaya ya Mbulu Mkoani
Manyara, SSP George Kyando akizungumza na jamii ya wafugaji wa kidatoga na
wairaqw wa Bonde la Yaeda Chini, ambao wana mgogoro wa muda mrefu, ambapo aliwaasa waache vurugu na kutekeleza dhana ya ulinzi shirikishi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mbulu Mkoani
Manyara, Fortunatus Fwema, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Hanang’ akiwaasa
jamii ya wafugaji wa kidatoga na wairaqw wa Bonde la Yaeda Chini, ambao wana
mgogoro wa muda mrefu kuwa waachane na vurugu na kufanya shughuli zao za kiuchumi za kifugaji na kilimo.
No comments:
Post a Comment