Tuesday, 18 February 2014

FARM AFRICA WAGAWA PIKIPIKI KWA MAOFISA UGANIMaofisa ugani 10 wa Wilaya za Babati na Mbulu, Mkoani Manyara, wamepatiwa pikipiki zenye thamani ya sh75 milioni, zitakazowasaidia kutoa huduma kwa jamii inaozunguka msitu wa Nou uliopo kwenye wilaya hizo.

Pikipiki hizo 10 zilitolewa kwa maofisa hao wa Serikali  mjini Babati  na shirika la Farm Africa, kupitia mradi wake wa usimamizi endelevu mfumo wa ikolojia wa msitu wa Nou, kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU).

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Babati Vijiji Zainab Mnubi alisema  maofisa ugani hao watatumia usafiri huo kwa lengo la kufanya kazi na watu 150,000 wa wilaya hizo wanaoishi kuuzunguka msitu huo.
Maofisa ugani 10 wa Wilaya za Babati na Mbulu, Mkoani Manyara, wamepatiwa pikipiki zenye thamani ya sh75 milioni, zitakazowasaidia kutoa huduma kwa jamii inaozunguka msitu wa Nou uliopo kwenye wilaya hizo.

Pikipiki hizo 10 zilitolewa kwa maofisa hao wa Serikali juzi mjini Babati  na shirika la Farm Africa, kupitia mradi wake wa usimamizi endelevu mfumo wa ikolojia wa msitu wa Nou, kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU).

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Babati Vijiji Zainab Mnubi alisema  maofisa ugani hao watatumia usafiri huo kwa lengo la kufanya kazi na watu 150,000 wa wilaya hizo wanaoishi kuuzunguka msitu huo.

“Mradi huu wa mwaka 2014-2016 utakapokamilika, pikipiki zitakuwa mali ya wakala wa msitu nchini (TFS) na halmashauri za wilaya zitawajibika kuhakikisha zinatumika kwa manufaa ya jamii na zinatunzwa vyema,” alisema Mbaga.

Alisema Farm Africa, TFS, Halmashauri za wilaya na maofisa wa Serikali katika kata wametia saini mkataba wa makubaliano kuhusu umiliki wa pikipiki na utendaji kazi kwenye kata husika kwa manufaa ya wakazi wa maeneo husika.   

No comments:

Post a Comment