Thursday, 6 February 2014

MZEE WA MIAKA 70 AUAWA MBEYA

MZEE MWENYE UMRI WA MIAKA 70 WENELA
SIBELA. MKAZI WA KIJIJI CHA MAGANJO ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUKATWA SHOKA KICHWANI NA KISOGONI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA NA KISHA MWILI WAKE KUTUPWA VICHAKANI. TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 05.02.2014 MAJIRA YA SAA 11:00HRS ASUBUHI WILAYA YA MBEYA VIJIJINI WAKATI MAREHEMU AKIWA NJIANI, CHANZO CHA MAUAJI KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.

No comments:

Post a Comment