Chama Cha
Mapinduzi jimboni Kalenga mkoani Iringa kimeanza rasmi mchakato wa
kumpata mgombea wa ubunge wa jimbo hilo. Uchaguzi mdogo unatarajiwa
kufanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Dk. William
Mgimwa.
Tayari
wanachama tisa wa chama hicho wamekwishachukua fomu kuonesha nia yao ya
kuingia katika kinyang'anyiro hicho. Wanachama hao ni Hafsa Mtasiwa,
Jackson Kiswaga, Godfrey Mgimwa, Edward Mtakimwa na Thomas Mwakoka.
Wengine ni Gabriel Kalinga, Msafiri Pamagil, Peter Mtisi na Grayson Kibasa.
Chama
hicho kitaendesha kura ya maoni siku ya Jumamosi tarehe 8 Februari. Kura
hiyo ni kwa ajili kupata jina la mgombea mmoja litakalowasilishwa
kwenye Tume ya Uchaguzi.
Tume ya Uchaguzi bado haijatangaza rasmi tarehe
ya uchaguzi jimboni humo.
No comments:
Post a Comment