Wachimbaji
wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilaya ya Simanjiro Mkoa wa
Manyara wametaka kuchukua tahadhari kwenye migodi yao wakati wakifanya shughuli
zao za uchimbaji madini hayo.
Inadaiwa
kuwa baadhi ya migodi hiyo ya Tanzanite haijafunikwa juu hivyo mchimbaji
anaweza kuteleza na kuanguka mgodini au mvua kubwa ikinyesha maji yanaweza
kuingia ndani ya mgodi na kusababisha athari kwa waanaApolo.
Wito
huo umetolewa na Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wa mkoa huo,
Mrakibu Msaidizi, Elisa Mugisha wakati akiongoza kikosi chaukaguzi wa kinga na
tahadhari ya moto na majanga mbalimbali kwenye migodi hiyo.
“Tumekagua
migodi zaidi ya 20 na baadhi yake tukatuka inamapungufu hivyo tumewaagiza
wakamilishe mapungufu yao ili wafanye shughuli zao kiuhakika ili madhara
yasiweze kujitokeza,” alisema Mugisha.
Alisema
pia walifika kwenye migodi ya wachimbaji wakubwa ya kampuni ya Tanzanite
Africa, TanzaniteOne na Kilimanjaro Mine ila walikagua migodi mitatu ya
TanzaniteOne na kubaini kuwa wamekidhi masharti ya uchimbaji madini.
“Sisi
tunatekeleza sheria za jeshi la zimamoto na uokoaji ya mwaka 2007 na kanuni ya
ukaguzi na vyeti vya usalama ya mwaka 2008 na marekebisho yake ya mwaka 2012,”
alisema Mugisha.
Pia,
kikosi hicho cha jeshi la zimamoto na uokoaji kilikagua vituo vya mafuta na
baadhi ya majengo ya biashara, makazi na taasisi mbalimbali za Serikali
zilizopo kwenye mji huo wa Mirerani.
No comments:
Post a Comment