Sunday, 7 July 2013

WATANO WAFA KWENYE MACHIMBO YA TANZANITE

                                                                                

Wachimbaji wadogo watano wa madini  ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani,Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara,wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na kifusi cha mchanga wakiwa mgodini. 

Katika tukio la ajali hiyo iliyotokea Julai 6 mwaka huu saa 1 jioni,kwenye machimbo ya madini ya Tanzanite Mirerani ,wachimbaji hao watano walifariki dunia papo hapo na mchimbaji mmoja akajeruhiwa kwenye tumbo na mbavuni.



Akithibitisha kutokea tukio hilo,Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara Kamishna Msaidizi,Akili Mpwapwa aliwataja waliofariki dunia ni Goodlove Zablon (35) na Ndekirwa Kitoi (33) wakazi wa Makiba Wilayani Arumeru.

Kamanda Mpwapwa aliwataja wachimbaji wengine waliofariki ni Jackson  Kavishe (45) mkazi wa Mirerani,Emmanuel John (33) mkazi wa Makiba na Emmanuel Joshua (40) mkazi wa Nkwoaranga wilayani Arumeru mkoani Arusha.

Alisema mchimbaji mwingine Sifael Simba (30) mkazi wa kijiji cha Maroroni wilayani Arumeru alijeruhiwa kwenye mbavu na tumboni ambapo amelazwa kwenye hospitali ya mkoa wa Arusha,Mount Meru.

No comments:

Post a Comment