Friday, 26 July 2013

MTUHUMIWA NAMBA MOJA



Janeth Jackson (32), mkazi wa Moshono, Arusha mke wa Jack Manjuru alifikishwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha, Devotha Kamuzora, akisomewa makosa mawili ya kula njama ya kutaka kumuua Simon Jackson Kaijage Manjuru ambaye ndiye mume wa Janeth.

RIP WILLY ONESMO MUSHI



Mchimbaji wa madini ya Tanzanite mwajiriwa wa kampuni ya TanzaniteOne ya Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Willy Onesmo Mushi (39) amefariki dunia baada ya kuuawa kwa kupigwa risasi ya bastola akiwa mgodini kwenye kampuni hiyo.

Saturday, 13 July 2013

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YAZURU MIRERANI

                                                                    

Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya kudumu ya Nishati na Madini, Mhe Anne Kilango Malecela (katikati) Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Mhe Richard Ndassa (kushoto) na Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kaskazini, Benjamin Mchwampaka wakiwa kwenye mkutano na wachimbaji wadogo wa Madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani.



Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya kudumu ya Nishati na Madini, Mhe Anne Kilango Malecela (katikati) akiongozwa na Mchimbaji wa madini ya Tanzanite (kushoto) Mohamed Karia ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Tan Youth Mining Ltd ambayo wachimbaji wadogo wanaiomba Serikali iifutie kodi na iipe kibali cha kuwasambazia zana za milipuko kwa bei nafuu.

                                                                                      

Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara, Mhe Christopher Ole Sendeka,akizungumza kwenye kikao cha Kamati ya Bunge ya kudumu ya Nishati na Madini, ilipotembelea wachimbaji wadogo wa madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani.

Sunday, 7 July 2013

MAMBO YA OBAMA

                                                                

                              Mambo ya Obama hayoo



         Rais wa Marekani Barack Obama na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete wakifurahia ngoma za utamaduni alipofanya ziara Tanzania Julai mosi mwaka huu



      Rais wa Marekani Barack Obama na Rais wa Tanzania    Jakaya Kikwete akisalimiana na baadhi ya watu  waliokuja kumpokea Obama alipofanya ziara Tanzania Julai mosi mwaka huu.