Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Manyara, Mosses Komba (wa pili kulia) akipokea bendera ya Chadema kutoka kwa aliyekuwa mjumbe wa kamati tendaji ya Chadema Wilaya ya Mbulu Stephano Geje wa mji mdogo wa Haydom ambaye yeye na wanachama wengine 10 walijiunga na CCM mjini Mbulu.
Mwenyekiti wa UVCCM
Mkoani Manyara, Mosses Komba akizungumza kwenye kikao cha baraza la UVCCM
Wilaya ya Mbulu katika ziara yake ya kutembelea wilaya hiyo.
MWENYEKITI
wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoani Manyara, Mosses Komba amesema ameanza mchakato wa kuhakikisha
Halmashauri za Wilaya za Mkoa huo zinawapatia vijana mikopo kupitia asilimia 5
ya mapato ya ndani.
Komba
aliyasema hayo mjini Mbulu wakati akizungumza kwenye kikao cha Baraza la UVCCM
la wilaya ya Mbulu.
Alisema
ameshatembelea baadhi ya halmashauri na kukutana na wakurugenzi watendaji hao
ambao wamempa utaratibu wa namna ya vijana hao kupata mikopo.
Aliwataka
vijana hao kujipanga kwenye hilo kwa kuanzisha vikundi ili mikopo itakapoanza
kutolewa wawe wamejiandaa kupitia umoja wao kwa ajili ya kufanikisha suala hilo
na kuagiza viongozi wa UVCCM wa wilaya hiyo kusimamia hilo.
"Nilipofika
hapa Mbulu nilipita kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya Chelestino Mofuga ili
kuzungumza naye aweke msukumo kwenye hilo nikamkosa kwani yupo likizo, lakini
nimeacha ujumbe juu ya hilo, hivyo vijana mtumie fursa hiyo," alisema
Komba.
Katibu
wa UVCCM wilayani Mbulu, Malkiori Pantaleo alisema jumuiya hiyo ina wanachama
15,477 kati yao wanaume ni 9,105 na wanawake ni 6,372.
Pantaleo
alisema hivi sasa wana mradi mmoja wa jengo na wamefanikiwa kurejesha ekari 12
za shamba la UVCCM lililokuwa na mgogoro tangu mwaka 2012 kwenye tawi la Getesh
kata ya Tumati.
Alisema
wapo kwenye mchakato wa ujenzi wa jengo la UVCCM la wilaya hiyo lililoungua kwa
moto Desemba 14 mwaka jana, ambalo lilikuwa linaingiza kipato kwenye jumuiya
hiyo.
Mbunge
wa jimbo la Mbulu mjini Paul Zacharia Isaay, amewataka vijana kupitia ilani ya
CCM na kutangaza mazuri yaliyofanywa na chama hicho.
Isaay
alisema vijana wakiwa wanajibu hoja kwenye vijiwe mitaani na katika mitandao
itasaidia kuweka ukweli hadharani pindi wapinzani wakipotosha maendeleo
yaliyofanyika.
Mbunge
wa jimbo la Mbulu Vijijini Flatei Massay amewataka vijana wajitokeze kugombea
nafasi mbalimbali pindi zikijitokeza ikiwemo uenyekiti wa vitongoji, vijiji,
mitaa, udiwani na ubunge.
Massay
alisema vijana wanapaswa kuchangamkia fursa hizo kwa kudhubutu kuchukua fomu na
kuacha woga kwani hata yeye alianza kuwa chipukizi, UVCCM na hivi sasa ni
mbunge.
So nice kijana hongera natamani kukuona nikirudi mkoani kwetu manyara by Rebeca Panga from babati magugu sarame karibu na huko kwetu jamani
ReplyDeleteSo nice kijana hongera natamani kukuona nikirudi mkoani kwetu manyara by Rebeca Panga from babati magugu sarame karibu na huko kwetu jamani
ReplyDeleteSo nice kijana hongera natamani kukuona nikirudi mkoani kwetu manyara by Rebeca Panga from babati magugu sarame karibu na huko kwetu jamani
ReplyDelete