Mkuu
wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka amemtuma mbunge wa jimbo la
Simanjiro Mkoani Manyara, James Ole Millya kumpelekea salamu aliyekuwa mgombea
urais wa Ukawa, Edward Lowassa kwa kumuunga mkono Rais John Magufuli, kwenye
kulinda rasilimali za Taifa.
Akizungumza
kwenye mazishi ya marehemu mama yake Raheli Sendeka yaliyofanyika kwenye Kijiji
cha Losokonoi Wilayani Simanjiro, Ole Sendeka alimtuma Ole Millya afikishe
salamu zake za shukrani kwa Waziri Mkuu mstaafu Lowassa.
Alisema
ni jambo zuri kwa Lowassa kuunga mkono jitihada za dhati za Rais Magufuli
kulinda rasilimali za nchi na baada ya kusoma magazeti kuwa Lowassa amempongeza
Rais Magufuli naye hana budi kumpongeza Lowassa kwa hilo.
"Nanyi
wabunge mkiwa bungeni muungeni mkono Rais wetu Magufuli anavyotetea rasilimali
za nchi ili madini yanayochimbwa yaweze kuwanufaisha watanzania waweze kupata
huduma zao za msingi kupitia madini yao, " alisema Ole Sendeka.
Pia,
aliwapongeza wabunge waliohudhuria mazishi hayo, akiwemo Mwenyekiti wa kamati
ya miundombinu Norman Sigala, mbunge wa jimbo la Babati Vijijini, Vrajlal
Jituson na Ole Millya, akiwataka waendeleze umoja kwa kutetea maslahi ya jamii
wakiwa Bungeni.
Askofu
wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya kaskazini kati,
Dk Solomon Masangwa alisema watanzania wanapaswa kuuenzi upendo walioachiwa na
Mungu.
Dk
Masangwa aliyasema japokuwa kuna msemo usemwao amani haipatikani ila kwa ncha
ya uwanja, watanzania wasikubali hilo kwa kudumisha umoja uliopo ili kuendeleza
amani iliyopo.
Naibu
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi William Ole Nasha, akitoa salamu za
rambirambi kwa niaba ya serikali alisema jamii inapaswa kumuenzi marehemu
Raheli Sendeka kwa kuiga yale yote mema aliyokuwa anayafanya kipindi cha uhai
wake.
"Mmoja
kati ya wajukuu wake Nailejileji Sendeka alisema bibi yake alimuasa kuwapenda
watu wote ambao Mungu amewaweka kwenye maisha kwa kuwathamini wenye uwezo na
wanyonge hivyo sisi sote tumuenzi kwa kuyatenda hayo," alisema Ole
Nasha.
Mbunge
wa jimbo la Simanjiro, James Ole Millya alisema wakati aliposhinda ubunge wa
jimbo hilo aliahidi kuwapenda na kuwapa ushirikiano wananchi wote wa wilaya
hiyo bila ubaguzi wowote ule.
"Mheshimiwa
mkuu wa Mkoa wa Njombe, niliahidi kutobagua watu kwenye uongozi wangu na hivi
ndivyo ninavyofanya ili kuweka pamoja jamii yetu ya jimbo la Simanjiro,"
alisema Ole Millya.
Mmoja
kati ya watoto wa marehemu huyo, Sumleck Ole Sendeka akisoma historia yake
alisema mama yao Raheli alizaliwa mwaka 1927 eneo la Oleng'iding'idata, kijiji
cha Lendanai wilayani Simanjiro.
Alisema
Raheli aliolewa na baba yao akiwa mke wa kwanza kati ya wake nane wa marehemu
baba yao mzee Olonyokie Ole Sendeka na alijaliwa watoto 12, kati yao saba wako
hai na watano walishafikisha, ameacha wajukuu 137,vitukuu 93 na kilembwe mmoja.
Alisema
marehemu alibatizwa mwaka 1971 KKKT mtaa wa Orkesumet usharika wa Naberera na
hadi anafariki alikuwa mshiriki mzuri wa maendeleo ya kanisa lake.
Alisema
marehemu alianza kusumbuliwa na tatizo la kisukari mwaka 2000 na kupatiwa
matibabu hospitali za KCMC, Mount Meru, Siima, St Thomas, Calvary Mirerani,
Losokonoi na Lendanai hadi alipoaga dunia saa 6 usiku, Juni 9 mwaka huu.
Mwenyekiti
wa kamati ya mazishi hayo mfanyabiashara Mathias Manga aliwashurukuru watu wote
walioshiriki kwa namna moja au nyingine kwa ajili ya kufanikisha shughuli zote
za mazishi hadi maziko.
No comments:
Post a Comment