Monday, 1 August 2016

MDAHALO WA MAENDELEO YA UCHUMI NA UWEKEZAJI KWENYE MADINI SIMANJIROMkurugenzi wa Shirika la Haki Madini, Amani Mustafa Mhinda akizungumza na wadau wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, kwenye mdahalo wa maendeleo ya uchumi na uwekezaji kwenye madini, juu ya ugatuaji na ugatuzi wa madaraka.Wadau wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakifuatili mdahalo wa maendeleo ya uchumi na uwekezaji kwenye madini uliondaliwa na shirika la Haki Madini.Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Albert Msole (katikati), Diwani wa Kata ya Mirerani Yohana Onyango, Mwenyekiti wa mtaa wa Twiga, Anthony Musiba na wadau wengine wa mji mdogo wa Mirerani, wakifuatali mdahalo wa maendeleo ya uchumi na uwekezaji kwenye madini, juu ya mpango wa uhamasishaji wa katika mapato ya madini, gesi asilia na mafuta.

No comments:

Post a Comment