Mkuu
wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona amewaagiza wote
waliovamia na kujikatia viwanja au kujenga kwenye eneo huru la usafirishaji
bidhaa nje (EPZA) waondoke na kubomoa kabla hawajaondolewa kwa nguvu.
Inadaiwa
kuwa vigogo watatu wa mji mdogo wa Mirerani, wamejenga nyumba za kuishi kwenye
eneo hilo na watu wengine zaidi ya 11 wamejimegea viwanja kiubabe na kujiandaa
kujenga ili hali mradi huo unatarajia kuanza kujengwa.
Akizungumza
juzi wakati akifungua maonyesho ya madini ya vito ya siku mbili yaliyofanyika
mji mdogo wa Mirerani, Kambona alisema mchakato wa kuwalipa fidia waliokuwa
wanamiliki eneo hilo upo tayari hivyo wavamizi hao waondoke.
Alisema
baada ya kuwalipa waliokuwa wamiliki wa eneo la EPZA, mchakato wa ujenzi
utaanza mara moja kwani kutajengwa kituo kikubwa cha biashara za kuuza nje
ikiwemo soko la madini ya Tanzanite litakalojengwa sehemu hiyo.
Hata
hivyo, alipongeza Wizara ya Nishati na Madini kufanya maonyesho hayo kwa mara
ya kwanza kwenye mji mdogo wa Mirerani, sehemu yanapopatikana madini ya
Tanzanite, kwani itasaidia kuboresha soko la madini katika eneo hilo.
“Ni
heshima kubwa tumepatiwa watu wa Simanjiro hususan mji mdogo wa Mirerani, hivyo
tutumie fursa hii kwa wachimbaji kuleta madini yetu kwenye maonyesho haya ili
kuboresha uchumi wetu,” alisema Kambona.
Mmoja
kati ya wachimbaji wa madini ya Tanzanite Saniniu Laizer alisema maonyesho kama
hayo yanachangia kutangaza madini hayo, kwani kuna baadhi ya watu wana dhana
potofu kuwa yanachimbwa nchi ya jirani.
“Kupitia
maonyesho haya tunaiomba serikali iboreshe zaidi sekta ya madini ya vito kwa
kuwapa kipaumbele wachimbaji wadogo kwani wana changamoto nyingi zinazowakabili
ikiwemo bei kubwa ya zana za milipuko,” alisema Laizer.
Kwa
upande wake, kaimu kamishna wa madini kanda ya kaskazini Elias Kayandabila
alisema maonyesho hayo yanafanyika kwa mara ya kwanza mji mdogo wa Mirerani na
yanatarajia kufanyika tena mwakani kwenye eneo hilo.
Kayandabila
alisema kupitia maonyesho hayo wafanyabiashara wadogo kwa wakubwa wa madini ya
vito ikiwemo Tanzanite, Tomarine ya kijani, Garnet ya kijani, Roadlite na
mengineno, watanufaika nayo kwa kuboresha masoko yao.
Maonyesho
hayo yameandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Nishati na Madini kanda ya ya
kaskazini na vyama vya wachimbaji madini (Remas), chama cha madalali wa madini (Tasgedo)
na chama cha wauzaji wa madini (Tamida).
No comments:
Post a Comment