LOWASSA AWASHUKURU WANANCHI WA MASASI KWA MAPOKEZI MAKUBWA ALIYOYAPATIA
Mgombea Urais wa Tanzania
wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward
Lowassa, akiwasili kwenye Uwanja wa Boma, Mjini Masasi Mkoani Mtwara,
kulikifanyika Mkutano wake wa Kampeni za kuomba ridhaa ya wananchi kugombea
nafasi, uliofanyika leo Septemba 22, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania
wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward
Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Masasi, Mkoani Mtwara, waliofikia
kusikiliza sera zake katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye
Uwanja wa Boma, leo Septemba 22, 2015. Ambapo amewashukuru wananchi wa Mji wa
Masasi kwa mapokezi makubwa waliyompatia.
Waziri Mkuu wa Zamani, Mh.
Fredrick Sumaye akizungumza machache na wananchi wa Jimbo la Masasi Mjini,
Mkoani Mtwara waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Boma, leo Septemba 22,
2015.CHANZO OTHMAN MICHUZI
Mgombea Urais wa Tanzania
wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward
Lowassa, akiwapungia mkono wananchi wa Mji wa Masasi, Mkoani Mtwara, muda mfupi
baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Boma, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni, leo
Septemba 22, 2015.
Uwanja wa Boma mjini
Masasi, palikuwa hapatishi pale Mgombea Urais alipowasili uwanjani
hapo.
Mgombea wa Ubunge
anaekubalika na wananchi wa Masasi kupitia Mwamvuli wa Chama cha Wananchi CUF,
Ismail Makombe (Maarufu kwa Jina la Kundambada), akizungumza machache na
wananchi hao waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Boma, leo Septemba 22,
2015.
Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa
kupitia Chama cha NLD, Dkt. Emmanuel Makaidi akiwa ameambatana na Mkewe,
wakiwasalimia wananchi wa Mji wa Masasi, Mkoani Mtwara leo Septemba 22,
2015.
Chademaaaaaa.........
Mgombea Urais wa Tanzania
wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward
Lowassa, akipokea karatasi ya Shairi kutoka kwa Msoma Mashairi, Mohamed Ally
(kushoto) mara baada ya kughani Shairi lake.
Magambo yenye jumbe mbali
mbali.
Sehemu ya Wananchi wa Mji
wa Masasi, Mkoani Mtwara wakiwa katika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa
Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh.
Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Boma, leo Septemba 22,
2015.
No comments:
Post a Comment