Maofisa ugani 10 wa Wilaya za Babati na Mbulu, Mkoani Manyara,
wamepatiwa pikipiki zenye thamani ya sh75 milioni, zitakazowasaidia kutoa huduma
kwa jamii inaozunguka msitu wa Nou uliopo kwenye wilaya hizo.
Pikipiki hizo 10 zilitolewa kwa maofisa hao wa Serikali mjini
Babati na shirika la Farm Africa,
kupitia mradi wake wa usimamizi endelevu mfumo wa ikolojia wa msitu wa Nou, kwa
ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU).
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya
Babati Vijiji Zainab Mnubi alisema maofisa
ugani hao watatumia usafiri huo kwa lengo la kufanya kazi na watu 150,000 wa
wilaya hizo wanaoishi kuuzunguka msitu huo.
Maofisa ugani 10 wa Wilaya za Babati na Mbulu, Mkoani Manyara,
wamepatiwa pikipiki zenye thamani ya sh75 milioni, zitakazowasaidia kutoa huduma
kwa jamii inaozunguka msitu wa Nou uliopo kwenye wilaya hizo.
Pikipiki hizo 10 zilitolewa kwa maofisa hao wa Serikali juzi mjini
Babati na shirika la Farm Africa,
kupitia mradi wake wa usimamizi endelevu mfumo wa ikolojia wa msitu wa Nou, kwa
ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU).
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya
Babati Vijiji Zainab Mnubi alisema maofisa
ugani hao watatumia usafiri huo kwa lengo la kufanya kazi na watu 150,000 wa
wilaya hizo wanaoishi kuuzunguka msitu huo.
“Mradi
huu wa mwaka 2014-2016 utakapokamilika, pikipiki zitakuwa mali ya wakala wa
msitu nchini (TFS) na halmashauri za wilaya zitawajibika kuhakikisha zinatumika
kwa manufaa ya jamii na zinatunzwa vyema,” alisema Mbaga.
Alisema
Farm Africa, TFS, Halmashauri za wilaya na maofisa wa Serikali katika kata
wametia saini mkataba wa makubaliano kuhusu umiliki wa pikipiki na utendaji
kazi kwenye kata husika kwa manufaa ya wakazi wa maeneo husika.